CMA YAHIMIZA WANANCHI KUJITOKEZA KUPATA ELIMU YA UTATUZI WA MIGOGORO YA KIKAZI.
Na: Mwandishi Wetu - Mbeya.
Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ambayo ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imewahimiza Wananchi kujitokeza katika banda la manesho ya wakulima (Nanenane) ili kupata elimu kuhusu utatuzi wa migogoro ya kikazi kwa njia ya Usuluhishi na Uamuzi.
Hayo yamebainishwa na Afisa Mfawidhi wa Tume hiyo wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Edgar Fungo Agosti 3, 2023 wakati wa maonesho hayo yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale Mkoani humo.
Amesema Migogoro ya kikazi inasuluhishwa kwa njia ya Usuluhishi na endapo ikishindikana inatatuliwa kwa njia ya Uamuzi.
“Ninahamasisha Wananchi kujitokeza kwa wingi katika banda letu ili waweze kupata uelewa kuhusu majukumu ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi katika kushughulikia migogoro ya kazi,” amesema.
CMA inashiriki maonesho hayo yaliyofunguliwa Agosti 1, 2023 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na yatafungwa Agosti 8 mwaka huo.
Post a Comment