MTAKA AITAKA CMA KUTOA MAFUNZO KWA WATUMISHI SEKTA YA UMMA NA BINAFSI ILI KUEPUSHA KESI ZINAZOJIRUDIA.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka ameitaka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kutoa mafunzo kwa wafanyakazi sekta ya umma na binafsi ili kuepusha kesi zinazojirudia mahali pa kazi.
Aidha, Mhe. Mtaka amesema kuwa migogoro na mivutano ambayo inajitokeza katika maeneo ya kazi inakwamisha utekelezaji wa majukumu, hivyo ameshauri tume hiyo kutoa mafunzo kuhusu utatuzi wa migogoro na taratibu za kufanya uamuzi wa kesi wanazopokea ili mahali pa kazi kuwe na tija.
Ameeleza hayo Agosti 4, 2023 alipotembelea banda la Tume ya Usuluhishi na Uamuzi katika maonesho ya siku ya wakulima (Nanenane) yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
“Fanyeni mapitio ya kesi zinazoletwa kwenu na muangalie makosa yanayo jirudia rudia ili mshirikiane na watumishi wa Utumishi kutoa mafunzo kwa wafanyakazi kazi katika sekta zote ili kuepusha kesi zinazojirudia rudia “ amesema Mtaka
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka akizungumza na watumishi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) alipotembelea banda hilo katika maonesho ya siku ya wakulima (Nanenane) yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) mara baada ya kutembelea banda la CMA katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya, Agosti 4, 2023.

Post a Comment