Header Ads

test

WATUMISHI HOUSING INVESTIMENTS YAELEZEA MIRADI YAKE KWA WANANCHI MAONESHO NANENANE

 

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV


WATUMISHI Housing Investiments (WHI) imetoa rai kwa watumishi wa umma pamoja na wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii kufika kwenye banda lao lililopo katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane yanayofanyika mkoani Mbeya.

Katika maonesho hayo Watumishi Housing Investiment imeebdelea kutoa taarifa ya miradi yao ya nyumba iliyopo Mwanza, Dodoma,Morogoro na Dar es salaam huku pia ikitoa elimu kuhusu uwekezaji kwenye mfuko wa uwekezaji wa pamoja unaoitwa mfuko wa Faida (Faida Fund).

Akizungumza kwenye Viwanja vya John Mwakangale, Meneja Masoko na Mawasiliano Raphael Mwabuponde Mwabuponde amesema lengo kubwa la kuwa kwenye maonyesho hayo ni kuwaelimisha wananchi kuhusu mifuko inayoendeshwa na WHI.

Ameitaja mifuko hiyo ni Mfuko wa nyumba unaitwa WHI REIT ambapo kwenye mfuko huo WHI wanajenga nyumba ambazo wanauziwa watumishi wa Umma, Diaspora pamoja na wanachama wa mfuko ya Hifadhi ya jamii, pia wanajenga majengo kwa ajili ya taasisi za Serikali.

Pia amesema WHI inaendedha mfuko wa uwekezaji wa pamoja unaoitwa mfuko wa Faida(Faida Fund) na lengo kubwa la mfuko huu likiwa ni kuongeza thamani ya Fedha ya muwekezaji au kukuza mtaji wa muwekezaji.

Amefafanua walengwa wa mfuko huo wa Faida (Faida Fund) ni wakulima,wafanyakazi wajasirimali, bodaboda,Mamalishe,wavuvi, taasisi za Serikali na zisizo za Serikali,NGO,VICOBA, Saccos pamoja na wanafunzi

"Kupitia mfuko huu napenda kusema kwamba mtu yeyote yule ambae anataka kujiunga kwaajili ya kuongeza thamani ya pesa yake anaweza kujiunga Kwa kupiga *152*00# arafu namba 1 malipo 6 WHI pia ataenda Faida Fund ambapo atakutana na kipengele ambacho kinahusiana na kutengeneza akaunti yake binafsi na kufuata maelekeza mpaka mwisho.

" Baada ya hapo utapewa namba ya kumbukumbu ya malipo (Control Number) ambayo ndiyo itatumika siku zote katika kununua vipande au kufanya uwekezaji, "amesema Mwabuponde.

Amesema muwekezaji atakuwa na uwezo wa kuwekeza Kwa kutumia tawi lolote la Benki ya CRDB, Wakala wa CRDB,Tigo pesa na Mpesa lakini pia Kwa kutumia Sim Banking

Aidha amebainisha kuwa huu mfuko gharama zake za uendeshaji ni nafuu kwa sababu unatumia mfumo wa malipo wa serikali GePG, pia hakuna gharama ya kujitoa au kujiunga kwenye mfuko huo.

Pia mfuko huo unamuwezesha mtu yoyote kukopa kwenye taasisi yoyote ya fefha kama vile banki Kwani uwekezaji wake ndio utakua dhamna yake ya mkopo huo.

Mwabuponde amesema WHI imeamua kuongeza nguvu katika kutoa elimu kwa wanafunzi na vijana wadogo ili kujenga uelewa zaidi kwa wanafunzi na vijana kwanza kuujua mfuko na "Faida Fund" na faida zake lakini pia kupandikiza elimu ya uwekezaji kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja.

Vile vile kutoa elimu kuhusu kununua nyumba kwa njia ya mikopo ya muda mrefu(mortgage loans) jambo ambalo tunadhani likikaa vizuri kwao litakuwa na faida kubwa kwa kizazi kijacho katika uwekezaji.

No comments