Header Ads

test

TAIFA STARS YAFUZU AFCON, REKODI MARA YA TATU

 


Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Tanzania imeweka rekodi ya kufuzu mashindano ya AFCON mara ya tatu baada ya mwaka huu wa 2023 kufuzu ugenini kwenye uwanja wa Annaba nchini Algeria baada ya sare ya 0-0 dhidi ya wenyeji hao Algeria hivyo kufikia alama nane zilizoivusha.

Mara ya kwanza, Tanzania ilifuzu mashindano hayo mwaka 1980 nchini Nigeria, wakati huo Taifa Stars ilikuwa chini ya Kocha Mkuu Joel Bendera. Mwaka 2019 Taifa Stars ilifuzu mashindano hayo ya AFCON nchini Misri chini ya Kocha Emmanuel Amunike.

Mara ya tatu kwenye uwanja wa Annaba, Algeria baada ya kuwalazimisha sare ya 0-0 wenyeji ikiwa ni mchezo wa Kundi F la kuwania kufuzu mashindano hayo. Uganda (The Cranes) wameshindwa kufuzu mashindano hayo licha ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Niger kwenye uwanja wa Marrakech, Morocco.

Katika Kundi hilo F, Algeria walishakata tiketi ya kufuzu mashindano hayo baada ya kuwa na alama 15 baada ya sare dhidi ya Stars (Tanzania) walifika alama 16, wakiwa kwenye nafasi ya kwanza. Stars wamemaliza nafasi ya pili wakiwa na alama nane, huku Uganda wakiwa na alama saba na Niger alama mbili pekee.

Taifa Stars watacheza mashindano hayo yanayoitwa AFCON 2023 ijapokuwa yatafanyika kati ya Januari na Februari 2024 nchini Ivory Coast.

No comments