HUDUMA ZA CT SCAN KUWANUFAISHA WANANCHI WA LINDI NA NCHI JIRANI
Na. WAF - Mtwara
Huduma za CT-Scan katika Mkoa wa Lindi zinakwenda kupunguza adha ya wananchi kusafiri kwa umbari mrefu kufuata huduma hizo Mikoa ya jirani.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu katika Mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan na wananchi wa Mkoa Lindi katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo.
Dkt. Mollel amesema kuwa faida za kuwa na huduma ya CT-Scan Mkoani humo imeishaonekana ambapo mpaka sasa zaidi ya watu 108 wamepata huduma hiyo katika Hospitali hiyo ambao walitakiwa kusafiri kwenda Mikoa ya jirani.
Sambamba na hilo Dkt. Mollel amesema kuwa jengo la wagonjwa wa dharura pia limekamilika na tayari vifaa vimeshasimikwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi wa Mkoa huo pamoja na nchi za jirani.
"Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu tunakushuru sana kwa uwekezaji mkubwa ulioufanya katika Sekta ya Afya hapa nchini mpaka sasa nchi jirani wanakuja kupata huduma za Afya Tanzania". Amesema Dkt. Mollel.
Post a Comment