Header Ads

test

SIMBACHAWENE AWAONYA WATUMISHI WANAOGUSHI UHAMISHO

Na Nasra Ismail, Geita

Watumishi wa serikali wameonywa kutokufanya udanganyifu ili kupata uhamisho kutoka katika vituo vyao vya mwanzo ili kupunguza uhaba wa watumishi katika maeneo husika.

Akizungumza na watumishi wa serikali katika halmashauri ya mji wa Geita Waziri wa nchi Ofisi ya Raisi Utumishi wa Umma na Utawala bora George Simbachawene alisema kuwa waliofanya udanganyifu tayari wameshajulikana na wanasubiri kuchukuliwa hatua.

Simbachawene aliongeza kuwa watumishi wengi wana uhamisho ambao ni wa uongo na utapeli na pia wameupata kwa kutoa rushwa.

Aidha Simbachawene aliwaasa watumishi ambao wamefanya udanganyifu ili kupata uhamisho warudi walikotoka kwani wasipofanya hivyo watafukuzwa kazi.

“tukigundua tutawarejesha walikotoka, na kwa maneno haya nayosema yule ambaye alihama kwa uhamisho wa uongo uongo na ameshindwa kuhamisha mshahara wake navoongea hapa arudi alikotoka vinginevyo atafukuzwa kazi” alisema Simbachawene.

No comments