DCEA, TAKUKURU WAZINDUA MONGOZO UTOAJI ELIMU DHIDI YA RUSHWA NA DAWA ZA KULEVYA
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)/wamezindua Mwongozo wa utoaji Elimu dhidi ya rushwa na dawa za kulevya kwa klabu za shuleni, vyuoni na nje ya Shule.
Aidha wamezindua Kampeni ya Kutokomeza Matumizi ya Dawa za kulevya na rRushwa katika jamii kupitia clabu za kupinga rushwa na dawa za kulevya Shuleni na Vyuoni huku ikielezwa kauli mbiu inasema Kataa Rushwa Kudhibiti Dawa za Kulevya.
Akizungumza leo Oktoba 4, 2023 jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa muongozo huo Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema Mei 26, 2023 mamlaka hiyo ya TAKUKURU waliingia makubaliano ya kushirikiana katika udhibiti na mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya na rushwa.
Amesema makubaliano hayo yalilenga kutumia klabu za kupinga rushwa zilizopo shuleni na vyuoni ili zitumike kutoa elimu kuhusu tatizo la dawa za kulevya na rushwa.
"Hatua hii itasaidia kuwajengea uwezo wanafunzi na wanaklabu kuwa waadilifu, wazalendo na wawajibikaji Zaidi na kuepuka vitendo vya rushwa na matumizi ya dawa za kulevya.
"Kutokana na makubaliano hayo, tuliamua kuandaa mafunzo kwa maofisa wetu wanaoshiriki katika kuzisimamia klabu hizo. Lengo kuu la mafunzo haya ni kuwa na ulewa wa pamoja kati ya maafisa wa TAKUKURU na DCEA...

" Na kupata namna bora na mbinu sahihi za kufikisha elimu katika klabu zinazopatikana mashuleni na vyuoni juu ya tatizo la dawa za kulevya na rushwa
Mafunzo haya yalianza rasmi Oktob 2 yanahitimishwa siku ya leo, "amesema.
Amefafanua tatizo la dawa za kulevya lina uhusiano wa karibu na tatizo la rushwa kwani yote ni makossa ya kupangwa na yanahitaji suluhu zinazofanana ambazo ni elimu sahihi kwa umma kuhusu madhara ya dawa za kulevya na rushwa katika jamii.
"Ni Imani yangu mafunzo haya yataleta tija kwa kuongeza kasi ya utoaji elimu, kufikia maeneo mengi katika ngazi za mikoa na wilaya, kuongeza nguvu kazi ya wakufunzi na kuwafikia wanafunzi wengi shuleni na vyuoni.
"Hivyo Taasisi zetu hizi mbili kwa pamoja tunazindua Kampeni ya Kutokomeza Matumizi ya Dawa za Kulevya na Rushwa katika jamii kupitia clabu za kupinga rushwa na dawa za kulevya Shuleni na Vyuoni. Kauli mbiu Mbiu ya Mpango huu ni Kataa Rushwa Kudhibiti Dawa za Kulevya.
Kamishina Jenerali Lyimo amesema lengo kuu la Kampeni hiyo ni kuelimisha umma kuhusu tatizo la rushwa na dawa za kulevya na kuuhamasisha ushiriki kukabili matatizo haya.
" Ni matarajio ya kampeni hii kuwa itawajengea uwezo wanafunzi-wanachama wa klabu za wapinga rushwa na wananchi kwa ujumla juu ya uelewa wa tatizo la rushwa na uhusiano wake na tatizo la dawa za kulevya."
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP Salum Hamduni
amesema taasisi hiyo na DCEA zilisaini mkataba wa makubaliano ya kikazi kwa madhumuni ya kuongeza wigo na nguvu ya kukabiliana na tatizo la rushwa na biashara pamoja na matumizi ya dawa za kulevya.
Amefafanua mkataba baina ya DCEA na TAKUKURU una maeneo mengi ya
ushirikiano na baadhi ya maeneo hayo ni kutoa mafunzo kwa watumishi wa DCEA na TAKUKURU, kubadilishana taarifa muhimu zitakazowezesha kukabili
biashara haramu ya dawa za kulevya, matumizi ya dawa haramu za kulevya.
Pia kudhibiti vitendo vya rushwa katika jamii;kushirikiana kutoa elimu kwa umma kwa kutumia njia na
majukwaa mbalimbali zikiwamo klabu za wapinga rushwa shuleni na vyuoni,kuhamasisha wanafunzi, vijana na jamii kwa ujumla
kutoshiriki vitendo vya rushwa na biashara na matumizi ya
dawa haramu za kulevya pamoja na kuchukua hatua kukabili
makosa haya.
"Ni furaha yangu kueleza tayari tumeanza utekelezaji wa makubaliano hayo ambapo kwa juma hili kuanzia Oktoba 2, hadi leo Oktoba 4, 2023 tulikuwa na mafunzo kwawatumishi wa DCEA na TAKUKURU wanaohusika na jukumu la
uelimishaji umma.
"Tunazindua kampeni
maalum ya uelimishaji.Mtakumbuka kati ya maeneo ya makubaliano ya ushirikiano huu ni kutoa elimu kwa umma kwa kutumia njia ya majukwaa zikiwamo klabu za wapinga
rushwa shuleni na vyuoni na ndio maana kampeni hii ni maalum kwa ajili ya uelimishaji mashuleni na vyuoni
"Jina la kampeni hii ni Tokomeza Rushwa na dawa za kulevya shuleni na vyuoni na kaulimbiu ya kampeni hii inasema Kataa rushwa kudhibiti dawa za kulevya‟.
" Ni matarajio yetu kampeni hii ikitekelezwa kwa ushirikiano
na wadau wote hapa nchini, ikiwemo waandishi wa habari na wadau wote wa sekta ya elimu, itachangia kuongeza uelewa wa wanafunzi, vijana na jamii kwa ujumla kuhusu ukubwa wa tatizo na madhila ya rushwa na dawa za kulevya." CP Hamduni.
Kamishna Jenerali Aretas Lyimo(kushoto) na Cp. Salum Hamduni ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU wakiwa wamezindua Mwongozo wa utoaji Elimu dhidi ya Rushwa na dawa za Kulevya kwa klabu za kupinga Rushwa za Kulevya Shuleni na Vyuoni.

Post a Comment