WAADHIMISHA WIKI YA UWT KWA KUSHIRIKI SHUGHULI ZA KIJAMII, KUTEMBELEA WENYE UHITAJI
Na Mwandishi Wetu.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake (UWT)Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Taifa Mariam Ulega amesema katika kuadhimidha Wiki ya UWT wameendelea kushiriki katika shughuli za mbalimbali za kijamii ikiwemo kuwatembelea wenye uhitaji.
kuhusu maadhimisho ya Wiki ya UWT Mariam Ulega amesema wao kama UWT T wanayo wiki yao ambayo ni maagizo kutoka kwa Mwenyekiti wao Taifa kwamba wafanye shughuli mbalimbali sambamba na kutembelea maeneo yanayotoa huduma za kijamii.
"Katika Wiki ya maadhimisho ya UWT tunahimizwa kutembelea shule , kwenye madawat ya kijinsia, hivyo ndio maana wao wamegawana katika makundi, kundi moja tumekuja hapa kundi lingine wameenda kwa watoto wa mgongo wazi.
"Kundi la lingnine la UWT limeenda kwa watoto yatima, lingine limeenda shuleni.Kwa hiyo nia na madhubumuni na lengo letu ni kuadhamidha wiki yetu lakini pia kuja kufanya matukio ya kijamii kama tulivyokuja kutembelea hospitali.
" Tumeweza kuona wanawake wenzetu ambao wamejifungua na wana watoto tayari lakini pia tutaenda kuangalia na wodi ya watoto.Hivyo basi tunawashukuru uongozi wa Hospitali kwa moyo wenu wa kukubali sisi kufika hapa."
Wakati huo huo jumuiya hiyo Mariam Ulega amekumbushwa mwakani ni Uchaguzi wa Serikali za mitaa itakaohusisha pia vijiji na vitongoji, hivyo wanawake wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi hizo.
Aidha wanawake wamekumbushwa kuwa mstari wa mbele katika kupambana na ukatili wa kijinsia."Mwenyekiti tuna wimbi kubwa la ukatili wa kijinsia linaendelea niwaombe viongozi wote nendeni katika wilaya zenu, kina mama wote nendeni katika wilaya zenu kuhakikisha ukatili wa kijinsia unatokomea nchini kwetu Tanzania.
"Nendeni mahakamani mfungwe vibwebwe mhakikishe mahakimu wanatoa hukumu kwa haki ,watanzania wote ni wamoja tupendane, tusiharibu maisha ya watoto wetu , niwaombe twendeni tukapambane na ukatili wa kijinsia."
Aidha ametumia nafasi hiyo kuelezea jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo ya wananchi huku akisisitiza Rais anafanya mengi makubwa katika hii nchi yetu.
" Mama halali asubuhi , mchana , jioni tuna muona anapambana kuhakikisha Tanzania inazidi kusonga mbele na kuwa na mafanikio makubwa sana."
Post a Comment