RAIS SAMIA AZINDUA SHULE ZILIZOJENGWA KWA MIRADI YA BOOST, SEQUIP NCHINI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan (kulia) na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa (kushoto), wakivuta pazia kuashia uzinduzi wa shule za awali, msingi na sekondari zilizojengwa nchi nzima kupitia Mradi wa Uhimarishaji Ufundishaji na Ujifunzaji (BOOST) na Mradi wa Kuimalisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) ambayo imegharimu Sh. Bilioni 230. Uzinduzi huo umefanyia leo Oktoba 15, 2023 Mkoani Singida.
...................................................
Na Dotto Mwaibale, Singida
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amezindua shule za awali, msingi na
sekondari zilizojengwa nchi nzima kupitia Mradi wa Uhimarishaji Ufundishaji na Ujifunzaji
(BOOST) na Mradi wa Kuimalisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) ambayo imegharimu Sh.
Bilioni 230.
Rais Samia amezindua Shule ya Msingi Imbele iliyopo Manispaa ya Singida na
Sekondari ya Mwanamwema iliyopo Halmashauri ya Singida kwa niaba ya Shule 302
zilizojengwa nchi nzima kupitia miradi ya BOOST na SEQUIP.
Akizungumza na wananchi baada ya kuzindua miradi hiyo Rais Samia Suluhu
Hassan alisema shule hizo zimejengwa Tanzania nzima na kuwataka wazazi
kuwasomesha watoto wao na kuhakikisha wanakwenda shuleni.
"Tulianza kujenga madarasa hayo kuanzia elimu ya awali tunataka
kumuandaa mtoto kuanzia akiwa na miaka mitatu hadi minne ombi langu kwenu
wazazi wenzangu ni kuhakikisha watoto wanakwenda shule," alisema Rais
Samia.
Rais Samia alisema amefurahishwa na watoto wa Shule ya Msingi Imbele wakati
wakimuimbia nyimbo na hiyo imetokana na
kujua matunda ya ujenzi wa shule hizo yanakwenda kuwanufaisha.
Aidha, Rais Samia alisema shule na miradi hiyo ni yetu hivyo inatakiwa
kulindwa na kutunza ili iendelee kuwanufaisha watoto watakaokuwa wanasoma
katika shule hizo.
Awali akisoma taarifa ya miradi hiyo Afisa Elimu Mkoa wa Singida,
Dkt.Elipidius Baganda alisema ujenzi wa miradi hiyo umekamilika kwa asilimia
100 na kuwa Halmashauri zote za Wilaya mkoani hapa kila moja ilipokea Sh.Milioni
493.6.
Leo Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea na ziara yake kwa kukagua barabara
yenye urefu wa kilometa 59.9 inayotoka Mkiwa, Itigi hadi Nolanga mkoani Mbeya
ambapo pia alifungua Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ikungi na Mkalama.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu alisema shule hizo
zimepunguza utoro kwa wanafunzi kutokana na kuwa jirani na kuwa hapo awali
walikuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu hivyo alitumia nafasi hiyo
kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa shule hizo.
Akizungumzia kuhusu kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha Polisi cha wilaya hiyo alisema kitasaidia kuuwe mji wa Ikungi salama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi huo.
Post a Comment