Header Ads

test

DKT. SHEIN AWATAKA WAHITIMU KUZINGATIA UADILIFU.

 

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Ally Mohammed Shein amewataka wahitimu wa elimu ya Vyuo vya juu kuzingatia nidhamu katika kuziendeleza taaluma zao kwa kuwa ndio msingi muhimu katika kuzifikia fursa mbalimbali za maendeleo.

Dkt. Shein ameyasema hayo katika Mahafali ya 22 ya Chuo Kikuu Mzumbe, baada ya zoezi la kuwatunuku vyeti wahitimu 4143, ambapo amesisitiza kuwa elimu lazima iende sambamba na nidhamu, bila nidhamu aliyepata elimu atapwaya.

"..zaidi ya hayo elimu lazima iende sambamba na nidhamu, nidhamu ni jambo kubwa sana, bila nidhamu aliyepata elimu atapwaya, atakuwa dhaifu, kwani sifa atakayopata ya elimu astashada, stashada au shahada yake itapwya" amesema Dkt. Shein

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Saida Yahya Othman na Mlau wa Chuo hicho wakatoa nasaha zao kwa wahitimu hao kuzingatia uadilifu mahala pa kazi.



Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Ally Mohammed Shein akizungumza wakati wa mahafali ya 22 ya Chuo Kikuu Mzumbe Novemba 023,2023 Kampasi Kuu Morogoro.











Maaandamano yakiendelea kuelekea kwenye eneo la mahafali.



Watumishi wa chuo hicho wakimsikiliza Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Ally Mohammed Shein.(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV)




















Sehemu ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe wakishangilia katika sherehe za mahafali ya chuo hicho yaliyohudhurishwa na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Ally Mohammed Shein.(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV)

No comments