MKUTANO WA PILI WA ACAT KUFANYIKA NCHINI RWANDA 2025
Na: Calvin Gwabara – Nairobi.
Washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa Teknolojia za Kilimo Barani Afrika wamezimia mkutano wa pili wa ACAT ufanyike Jijini Kigali ncnhini Rwanada.
Hilo limesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Teknolojia za Kilimo Afrika (AATF) Dkt. Canisius Kanangire wakati akisoma maazimio ya mkutano huo kwa niaba ya washiriki wote zaidi ya 500 kutoka nchi mbalimbali za afrika na nje ya Afrika.
“Kwa pamoja wadau wa mkutano huu ambao utakuwa unafanyika kila baada ya miaka miwili tumekubaliana kukutana tena kukutana tena mjini Kigali, Rwanda kuanzia tarehe 19 - 23 Mei, 2025 ili kutathmini yale ambayo tumekubaliana kuyafanya kila mmoja wetu na wadau” Alieleza Dkt. Kanangire.
Aidha amesema wadau wamepitisha ACAT kuwa kongamano la kila baada ya miaka miwili katika bara litakaloonyesha teknolojia na ubunifu zinazoibukia, uanzishaji wa mitandao na kufungua ufikiaji wa teknolojia na uhauwilishaji wake.
Wametoa wito kwa Umoja wa Afrika (AU) kutambua na kushirikisha taasisi ambazo zimefanya vyema katika nyanja ya maendeleo na usambazaji wa Teknolojia za Kilimo kama vile AATF kama mshauri wao wa kiufundi katika masuala ya Teknolojia ya Kilimo.
Pia maazimio hayo yametaka kurejelea hitaji la uwekezaji katika shughuli zinazounga mkono ufanyaji biashara na upitishaji wa teknolojia za kilimo ikiwa ni pamoja na kuimarisha huduma za ugani, kuzalisha bidhaa zenye ufanisi na kuondoa vikwazo vya Kitarifuna zisizo za tarifu.
Pia wametoa wito wa kupunguzwa athari hasi za ongezeko mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) zinazopinga uvumbuzi wa kiteknolojia wa riwaya ikijumuisha viumbe vilivyobadilishwa vinasaba (GMOs) barani Afrika kupitia majadiliano yenye kujenga na ushirikishwaji wa malengo, unaoungwa mkono na ushahidi wa kisayansi badala ya upotoshwaji usio na ushahidi.
Post a Comment