Header Ads

test

TANZANIA INASAIDIA WAKULIMA KUPAMBANA NA MADILIKO YA TABIA NCHI

2/11/2023 Nairobi Tabianchi


Tanzania kupitia wizara yake ya kilimo kwa kushirikiana na Wadau
wengine imekuwa ikitekeleza mbinu mbalimbali za kuhimuli athari za
mabadiliko ya tabia nchi kwa wakulima na wafugaji nchini.

Hayo yameeezwa na Bw. Kamwesige Mujuni Mtembei ambaye ni Afisa
mwandamizi kutoka Wizara ya Kilimo nchini Tanzania wakati akizungumza
kwenye mjadala uliohusu juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali
katika kusaidia jamii kukabiliana na athari za hizo kwenye mkutano wa
teknolojia za kilimo barani Afrika unaoendelea Jijini Nairobi Nchini Kenya
na kukutanisha mamia ya Wadau wa kilimo Afrika na duniani.

“Tanzania ni kati ya nchi zilizoathiriwa sana na mabadiliko ya tabia nchi
kama vile Ukame,Mafuriko katika baadhi ya maeneo na kupanda kwa
viwango vya joto hivyo Wizara kupitia mikakati na miongozo ya kilimo
himilivu inawaelimisha wakulima namna ya kuboresha kilimo na ufugaji
kwa ili kupata tija” alieleza Bw. Mtembei.

Aliongeza “ Kwa kutambua kuwa vijana na wakina Mama ni waathirika
zaidi wa tatizo hili Serikali inaendesha program ya Jenga Kesho Bora (BBT)
ambayo inalenga kuimarisha upatikanaji wa mashamba yenye
miundombinu ya umwagiliaji na upatikanaji wa mitaji na masoko kwa
wakina Mama na vijana”.

Ameongeza kuwa Wizara inaendelea kuboresha miundombinu ya
umwagiliaji kuhamasisha utafiti na uzalishaji wa mbegu bora sambamba na
kuongeza bajeti ya utafiti wa mbinu na teknolojia mbalimbali za kilimo
himilivu cha mabadiliko ya tabia nchi.

Afisa huyo mwandamizi wa Kilimo amesema Wizara inaendesha miradi ya
kutoa pembejeo za ruzuku ili kuwezesha wakulima kumudu matumzi ya
pembejeo katika kuongeza tija.

Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Kenya
kupitia Wizara yake ya Kilimo na maendeleo ya Ufugaji na Taasisi ya
Teknolojia za Kilimo Afrika AATF na unawakutanisha wadau wa kilimo
kutoka afrika na pande zote za Dunia.
Bw. Kamwesige Mujuni Mtembei ambaye ni Afisa mwandamizi kutoka Wizara ya Kilimo nchini Tanzania wakati akizungumza kwenye Mkutano wa ACAT.Mchokoza mada wa mjadala huo ambaye ni Makamu Mkurugenzi wa misheni wa USAID nchini Kenya Bi.Sheila Roquitte akichokoza mada.
Wadau wa Kilimo kwenye mkutano huo wakifuatilia na kuchangia mjadala wa mabadiliko ya tabia nchi barani Afrika.



wadau wa mkutano huo wakifuatilia mjadala huo.

No comments