Header Ads

test

TT SECURITY INAVYOCHANGIA AJIRA KWA VIJANA KUPITIA SEKTA YA ULINZI

 

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ulinzi ya TT Security, Beatrice Eugen akizungumza katika kikao na viongozi na wasimamizi wa vituo mbalimbali kilichofanyika Kurasini Dar es Salaam.

Meneja Mkuu wa kampuni ya Ulinzi ya TT Security, Maitalya Mwise, akifafanua namna kampuni hiyo inavyochangia mapato ya serikali kwa kuhakikisha inalipa kodi zote za nchi kwa mujibu wa miongozo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Msimamizi wa Lindo la Sea View Apartments, Felister  Masulube, akizungumza katika kikao cha viongozi na wasimamizi wa TT Security kilichofanyika, TEC Kurasini Dar es Salaam, mwanzoni mwa wiki Dar es Salaam,

Sehemu ya walinzi wa kampuni ya TT Security waliohudhuria kikao cha viongozi na wasimamizi wa kampuni ya ulinzi ya TT Security wakifuatilia kwa makini mada iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TT Security, Beatrice Eugen (hayupo pichani) kuhusu maadili.

KAMPUNI binafsi ya ulinzi ya TT Security inaona fahari kuchangia juhudi za serikali kuwaletea wananchi maendeleo kupitia ukusanyaji kodi na kusaidia kukabili tatizo la ukosefu wa ajira kwa kuajiri vijana katika tasnia ya ulinzi.

Meneja Mkuu na Meneja wa Operesheni wa TT Security, Maitalya Mwise na Kulwa Mutabazi walibainisha hayo katika kikao cha kutathmini changamoto na mafanikio ya kampuni hiyo kwa mwaka 2023 kilichofanyika Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini, Dar es Salaam kikihusisha wasimamizi wa vituo katika mikoa mbalimbali nchini.

Alisema kampuni hiyo imekuwa wakala mzuri wa kukusanya na kuwasilisha kodi serikalini kutokana na vyanzo mbalimbali ikiwamo mishahara ya wafanyakazi (PAYE) na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa wastani wa Sh milioni 20 kila mwezi.

“Tunajua ulipaji kodi sahihi ndio unaoisadia serikali kutoa huduma mbalimbali za jamii zikiwamo wa elimu, afya, miundombinu, umeme na maji hivyo, ni wajibu wetu kuunga mkono juhudi hizi,” alisema Mwise.

Akitoa taarifa kuhusu kampuni hiyo kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kwa mwaja jana, Meneja Operesheni wa TT Security, Kulwa Mutabazi alisema walifanikiwa kuzuia matukio 30 ya wizi na kukamatwa watuhumiwa kadhaa ambao baadhi kesi dhidi yao zimefunguliwa.

“Kwa mwaka jana tulikabidhi malindo matatu makubwa baada ya miradi kukamilika na lingine, mteja alishindwa kutekeleza makubaliano ili kazi ifikie kiwango chetu cha utoaji huduma bora,” alisema.

Alitaja baadhi ya malindo waliyokabidhi salama baada ya mradi kukamilika kuwa ni pamoja na Daraja la Wami (Mkoani Pwani) na Stendi Kuu ya Mabasi ya Magufuli maarufu, Mbezi iliyopo Dar es Salaam na kampuni ya Kichina ya Highland International (Dar es Salaam, Dodoma na Mtwara).

Kwa mujibu wa Mutabazi, mwaka jana TT Security inayotoa huduma za ulinzi kwa kutumia askari, askari na mbwa pamoja na askari na bunduki kutegemea hali na mahitaji ya lindo, iliajiri vijana 195 katika tasnia hiyo inayoto.

“Tunatimiza jukumu letu la ulinzi kwa weledi mkubwa kulinda watu na mali zao sambamba na kuhifadhi wa mali hizo zisiathiriwe vibaya na mvua, jua upepo au jambo lolote baya,” alisema Mwise.

Mkurugenzi Mtendaji wa TT Security, Beatrice Eugen alihimiza viongozi na wasimamizi hao wa vituo kuhakikisha wanaendelea kuhakikisha waajiriwa wote wanaendeleza uaminifu, uadilifu na utoaji wa huduma bora kwa wateja.

“Kazi ya ulinzi yaani kuwapa watu usalama wao na mali zao; ni kazi ya Mungu; ni mwito, lazima ifanyike kwa uadilifu, uaminifu na kwa kujitoa zaidi na hata inapotokea kunahitajika ukamataji kwa mtuhumiwa, askari wetu lazima wazingatie ukamataji salama sambamba na sheria za nchi,” alisema Eugen.

Kwa upande wake, Beatrice alitaja nguzo tano zinazoongoza kampuni hiyo kuwa ni uaminifu, uadilifu, unadhifu, utii na huduma bora.

“Ni muhimu askari kuwa na uhusiano na ushirikiano bora na wanajamii wanaokuzunguka kupitia ulinzi shirikishi, lakini pia kuzingatia kuwa wahalifu hasa wezi, wengi hutumia fursa ya mazoea kufanya uhalifu,” alisema.

No comments