Header Ads

test

RIDHIWANI AKABIDHI PIKIPIKI KWA MAOFISA UGANI CHALINZE

 Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amekabidhi pikipiki 6 kwa Maafisa Ugani wa Halmashauri wa Halmashauri ya Chalinze ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuwapatia Vitendea kazi Watumishi kwenye sekta ya Kilimo na Mifugo .

Akikabidhi Pikipiki hizo , Ridhiwani ameeleza, zimetolewa na Serikali Kuu kupitia Wizara ya Kilimo na zinalenga kuwawezesha  maafisa Ugani kuweza kufika katika maeneo na kwa wenye uhitaji ili kuboresha sekta ya kilimo ."Kugawiwa kwa pikipiki hizi kunafanya maafisa ugani waliopewa vifaa hivi kufika 14 kati ya kata 16 za Halmashauri hii".

Halmashauri ya Chalinze ni moja kati ya Halmashauri zinazoongoza kwa kilimo katika eneo la Mashariki ya Tanzania.





No comments