Header Ads

test

DC LUSHOTO ATANGAZA KUSOGEZWA MBELE USAMBARA TOURISM FESTIVAL

Na Ashrack Miraji Lushoto Tanga 


MKUU wa Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga Jafar Kubecha amewaomba radhi wananchi na wageni wote waliotarajia kudhuhuria katika  tamasha la  kitalii la "Usambara Tourism Festival" lenye lengo la kukuza uchumi hasa kwenye sekta ya utalii wilayani hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Wilaya Kubecha amesema tamasha hilo lililopagwa kufanyika  Julai  25 hadi 27 mwaka huu sasa limesogezwa mbele kutokana  na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao,hivyo tamasha litafanyika Septemba 6 hadi  7  mwaka huu.

"Nitumie fursa  hii kuwapa pole wananchi na wageni wetu ambao tuliwatarajia kushiriki kwenye tamasha letu kuja kujionea vivutio mbalimbali vya kitalii na majengo makubwa ambayo yalijegwa na mjerumani hususani jengo la Mkuu wa Wilaya ya Lushoto" amesema Kubecha.

 

No comments