Header Ads

test

Alliance One yajenga viwanja vya shule ya msingi gharama ya 241m/-

 


Na Mwandishi Wetu Morogoro


Serikali imepokea viwanja vitatu vya michezo pamoja na njia maalum ya riadha, vilivyojengwa kwa msaada wa kampuni ya tumbaku ya Alliance One(AOTL), vilivyopo katika shule ya msingi Kingolwira manispaa ya Morogoro kwa jumla ya gharama ya milioni 241.   

Akipokea msaada huo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sanaa , Utamaduni na Michezo, Dr Suleiman Serera amesema viwanja alivyokabidhiwa ni kiwanja cha mpira wa miguu, kiwanja cha mpira wa pete na kiwanja cha mpira wa kikapu, ambapo kampuni hiyo imetoa msaada huo kupitia sera yake ya misaada kwa jamii.

"Msaada huu unaenda sambamba na Sera ya Taifa ya michezo ya mwaka 1995, pamoja na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kufanya kazi kwa karibu na taasisi binafsi katika kuwaletea wananchi maendeleo," amesema.

Amesema msaada huo umeendana na mpango wa serikali wa kujenga miundombinu ya viwanja kwenye shule 56 nchi nzima, lengo likiwa kuweka mazingira bora ya michezo kwa watoto wa shule ya msingi na sekondari kupitia mashindano yao ya Umitashumta, lengo likiwa kuandaa vipaji kwa jili ya kucheza kombe la dunia mwaka 2030.

Dr Serera ameishukuru kampuni hiyo kwa ujenzi wa viwanja ambapo sasa wameboresha mazingira yatakayosaidia kuibua vipaji walivyo navyo watoto mashuleni na hivyo wataweza kujiendeleza kirahisi kwani michezo ni ajira.

"Tukitaka watoto wetu wafike mbali katika mambo ya utamaduni,sanaa na michezo ni lazima tuboreshe mazingira yao na hapa nawapongeza Alliance One kwa kulichukua hili na kulitendea kazi kwa niaba ya serikali,"amesema na kuongeza kuwa ujenzi huo unaungana na juhudi za serikali kujenga na kuendeleza viwanja vya michezo nchini kikiwemo cha Arusha na Dodoma kwa ajii ya maandalizi ya Afcon mwaka 2027.

Amevisifu viwanja hivyo kwamba vimejengwa kwa hadhi ya kimataifa na kwamba vimewekewa miundombinu ya maji ya umwagiliaji majani ili yasikauke,badala yake yawe na kijani kibichi mwaka mzima na hivyo kuweza kuiingizia kipato shule kutoka kwenye timu kubwa kubwa za michezo zinazopiga kambi zao mkoani Morogoro kuvikodidha kwa ajili ya kufanyia mazoezi.
"Nimeona mmejengewa tenki la maji lenye uwezo wa kutunza lita 30,000 wakati mmoja, lakini matumizi yenu hapa shuleni ni lta 5000 pekee,hivyo ziada hiyo itaenda kufanya utuzani wa mazingira ya shule ikiwemo mazingira ya viwanja vya michezo," alisema.

Amesema kuwa ameambiwa siyo mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kutoa msaada shuleni hapo, kwani imekuwa ikitoa misaada mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa, matundu ya vyoo,kuchimba kisima cha maji vikiwa vimegharimu mamilioni ya fedha.

"Niwapongeze sana Alliance One kwa ufadhili huu, kwani natambua kwamba ziko taasisi nyinyi ambazo zinapata faida na zinafanya mambo mengine na hawarudishi ipasavyo kwa jamii kama ninyi mlivyotoa kwani kutoa ni moyo siyo kwamba ni utajiri,"amesema na kuongeza kuwa amekoshwa na msaada wa madarasa ya awali shuleni hapo ambayo yana mazuria mazuri.

Msemaji wa Kampuni hiyo Wakili John Magoti amesema gharama za ujenzi huo wa viwanja vitatu vya michezo umgharimu shilingi 241, fedha ambazo zimelipwa kwa mkandarasi mzawa ambaye amefanyakazi kwa wakati.

“Tumetoa msaada huu tunaoukabidhi leo, lengo likiwa ni kuendeleza michezo kwa watoto, kwani tunaamini kwamba baada ya masomo ya darasani, kuna umuhimu kwa kwajengea watoto afya ya akili kupitia michezo aina mbalimbali inayochezwa kwenye mazingira mazuri,” amesema.

Amesema kampuni yake ina imani kwamba viwanja hivyo vitasaidia kuibua vipaji vingi katika michezo, na hivyo kusaidia kupata wachezaji maarufu wenye majina makubwa hapa nchini.

Akipokea msaada huo Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Emmanuel Mkongo ameipongeza kampuni hiyo kwa msaada wa viwanja hivyo vitatu, huku akiahidi kuvitunza viwanja hivyo kwa hali na mali ili vichangie kuikuza sekta ya michezo nchini.

“Kwakuwa sekta ya michezo muhimu sana imesisitizwa na imepewa msisitizo na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan, sisi wana Morogoro hatutamuangusha Rais wetu kwa kutekeleza maagizo yake kuhusu michezo hasa baada ya kupata viwanja hivi,” amesema.

Kaimu Mkurugenzi wa Aliance One Blasius Lupenza ambaye pia ni Mkurugenz wa Rasilimali watu kwenye kampuni hiyo amesema misaada wanayoitoa kwenye shule hiyo ni ya ujirani mwema wamekuwa wakiifanya kwa maika mingi.

“Shule hii ni majirani zetu, tunaposema rasilimali watu siyo kitu kingine, ni hawa wanafunzi ambao sasa tunawaandaa ili waje kuwa vijana bora na wafanyakazi bora ili taifa liweze kunufaika nao, maana baada ya muda fulani baada ya masomo yao watakuja kuajiriwa na kampuni yetu,” amesema.

Ameahidi kwamba kampuni yake itaendelea kutoa misaada kwa jamii kotekote kule ambako wanafanya kazi za kitumbaku ikiwemo wilaya za Sikonge,Uyui na Urambo mkoani Tabora, Kasulu na Kibondo mkoani Kigoma,Kahama na Ushetu mkoani Shinyanga na Serengeti Mara, ambako kampuni inatenga kati ya shilingi milioni 400 hadi 500 kila mwaka kwa ajili ya misaada kwa jamii.

Amesema kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kampuni hiyo imetoa misaada mbalimbali shuleni hapo iliyogharimu jumla ya shilingi milioni 176.

Ameitaja misaada hiyo kuwa ujenzi wa darasa la awali lililogharimu shilingi milioni 21, ujenzi wa vyoo vya waalimu vya kisasa pamoja na chumba maalum cha watoto wa kike wanaovunja ungo(sick bay) kwa gharama ya shilingi milioni 48.3.

“Msaada mwingine ni ukuchimba kisima kirefu cha maji na ufungaji wa umeme jua chenye uwezo wa kuvuta lita 30,000 za maji kilichogharimu shilingi milioni 13.7, pamoja na ujenzi wa jiko la shule na bwalo la chakula kwa gharama ya shilingi milioni 45,” amesema.
Naibu Katibu wa Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni, Dk Suleiman Serera(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Kingolwira iliyopo Manispaa ya Morogoro, mara baada ya kuzindua viwanya vitatu ambavyo ni kiwanja cha soka,kiwanja cha mpira wa kikapu na kiwanja mpira wa netiboli vilivyojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya tumbaku ya Alliance One.  
Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Mogororo Emmanuel Mkongo(wa tatu Kulia), Kaimu Mkurugenzi MKuu wa AOTL, Blasius Lupenza(wa pili kulia) na Msemaji wa Kampuni hiyo Wakili John Maagoti(wa pili kushoto) na Mwalimu mkuu wa shule hiyo, John Fulana(kushoto)
Naibu Katibu wa Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni, Dk Suleiman Serera akirusha mpira wa kikapu na kufunga goli kuashiria uzinduzi wa viwanja vitatu vya michezo ambavyo ni  cha kikapu,soka na netiboli vilivyojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya Alliance One(AOTL) kwenye shule ya msingi Kingolwira Manispaa ya Morogoro.Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Mogororo Emmanuel Mkongo(wa pili Kulia), Kaimu Mkurugenzi MKuu wa AOTL, Blasius Lupenza(wa tatu kulia) na Msemaji wa Kampuni hiyo Wakili John Maagoti(wa nne kulia).
Naibu Katibu wa Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni, Dk Suleiman Serera, akipiga penati na kufunga goli kuashiria uzinduzi wa viwanja vitatu vya michezo ambavyo ni  cha kikapu,soka na netiboli vilivyojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya Alliance One(AOTL), kwenye shule ya msingi Kingolwira iliyopo Manispaa ya Morogoro.Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Mogororo Emmanuel Mkongo(wa pili Kushoto), Kaimu Mkurugenzi MKuu wa AOTL, Blasius Lupenza(wa pili kulia) na Msemaji wa Kampuni hiyo Wakili John Maagoti(kulia).
Naibu Katibu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Suleiman Serera akikata utepe kuashiria uzinduzi wa viwanja vitatu vya michezo ambavyo ni  cha kikapu,soka na netiboli vilivyojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya Alliance One(AOTL) kwenye shule ya msingi Kingolwira Manispaa ya Morogoro.Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Mogororo Emmanuel Mkongo(wa pili Kushoto), Kaimu Mkurugenzi MKuu wa AOTL,Blasius Lupenza(wa pili kulia) na Msemaji wa Kampuni hiyo Wakili John Maagoti(kulia).
Naibu Katibu wa Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni, Dk Suleiman Serera akipanda mti wakati wa sherehe ya uzinduzi wa viwanja vitatu vya michezo ambavyo ni  cha kikapu,soka na netiboli vilivyojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya Alliance One(AOTL) kwenye shule ya msingi Kingolwira Manispaa ya Morogoro.Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Mogororo Emmanuel Mkongo(wa nne Kushoto), Kaimu Mkurugenzi MKuu wa AOTL, Blasius Lupenza(wa tatu kulia) na Mwalimu Mkuu shule hiyo John Fulana (kulia)
Naibu Katibu wa Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni, Dk Suleiman Serera(mwenye miwani mieusi) akiwa katika picha ya pamoja wenyeji na wageni kwenye sherehe ya uzinduzi wa viwanja vitatu vya michezo ambavyo ni  cha kikapu,soka na netiboli vilivyojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya Alliance One(AOTL) kwenye shule ya msingi Kingolwira Manispaa ya Morogoro.Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Mogororo Emmanuel Mkongo(kulia Dk Serera), Kaimu Mkurugenzi MKuu wa AOTL, Blasius Lupenza(kushoto kwa Dk Serera) na Msemaji wa AOTL(wa  pili kushoto kwa Dk Serera). 

No comments