Header Ads

test

WAZIRI MKUU ATOA MAELEKEZO KWA WADAU KUDHIBITI BIDHAA BANDIA

Na Mwandishi Wetu


WAZIRI Mkuu Kasimu Majaliwa ametoa maagizo kwa wadau wa udhibiti wa bidhaa bandia nchini kuzingatia sheria ya alama na kushirikiana na Tume ya Ushindani (FCC), kudhibiti bidhaa bandia kukuza biashara na uwekezaji nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri  Mkuu Majaliwa aliyekuwa mgeni rasmi ,Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe pia amewataka wamiliki wa nembo nchini kuhakikisha wanafuatialia bidhaa zao na kuziwasilisha FCC pale wanapogundua wafanyabiashara wanatumia bidhaa zao zilozobadilishwa uhalisia.
 maagizo maane 

"Endeleeni kutoa elimu kwa walaji kuhusu  athari za bidhaa bandia, Wakala wa Forodha, kushirikiana na FCC kuhakikisha bidhaa bandia haziingii kupitia bandari na sehemu za mipakani.

"Pia wafanyabiashara hakikisheni mnazingatia sheria ya alama za bidhaa ya mwaka 1993, iliyofanyiwa marekebisho inayokataza kuingiza, kuuza na kuhifadhi kwani adhabu yake ni kifungo na faini,"  amesema.

Ametumia nafasi hiyo kuwataka FCC kushirikiana na taasisi zingine kudhibiti bidhaa hizo kuhakikisha wawekezaji wanakuwa na imani, katika ukanda wa Afrika Mashariki (EAC) na ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

"Udhibiti wa bidhaa bandia sio jambo la mtu mmoja, hivyo washirikiane wote kuhakikisha wanadhibiti suala hilo ambapo watasababisha kuwa na mafanikio zaidi kuvutia wawekezaji."

Pamoja na hayo Waziri Mkuu kupitia Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara FCC kuongeza wigo wa mashirikiano, mashirika mbalimbali ya kimataifa  ya biashara na udhibiti wa bidhaa feki kuelimisha wadau kuhusu madhara ya bidhaa bandia.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe akisoma hotuba yake wakati wa maazimisho ya siku ya kudhibiti bidhaa bandia Duniani katika ukumbi wa Mlima City Jijini Dar es Salaam leo tarehe 18 Julai 2024.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) William Erio akizungumza wakati wa  maazimisho ya siku ya kudhibiti bidhaa bandia Duniani katika ukumbi wa Mlima City Jijini Dar es Salaam leo18 tarehe Julai 2024.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hassan Bomboko akizungumza wakati wa  maazimisho ya siku ya kudhibiti bidhaa bandia Duniani katika ukumbi wa Mlima City Jijini Dar es Salaam leo 18 tarehe Julai  2024.


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe akiwa ameambata na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) William Erio pamoja na watumie wa (FCC) alipotembelea mabanda wakati wa maazimisho ya siku ya kudhibiti bidhaa bandia Duniani katika ukumbi wa Mlima City Jijini Dar es Salaam leo tarehe 18 Julai , 2024.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV) 

SEHEMU ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe (hayupo pichani)



Mkutano ukiendelea.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV) 




Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,Exaud Kigahe akia kwenye picha ya pamoja.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV) 





.                    (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV) 

No comments