Header Ads

test

Kampuni ya Sun king yafungua maduka jijini Dar na mtambo wenye uwezo mkubwa wa matumizi ya umeme jua

 


Kampuni ya Sun King imefungua maduka matatu ya kisasa ya vifaa na mtambo  mpya wenye uwezo mkubwa wa kuwezesha matumizi ya  umeme jua katika juhudi za kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania za nishati safi , salama na kutuza mazingira hapa nchini.

Akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa maduka hayo ya kisasa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam mgeni rasmi kwenye ufunguzi huo, Msanii Mrisho Mpoto, alisema kwamba vifaa na mitambo ya kampuni hiyo ni mbadala mkubwa wa majenereta ambayo kwa kiasi kikubwa yanaleta moshi na makelele kwenye miji na kuchafua mazingira.

“Hizi ni jitihada za kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika nishati safi na salama na siku ya leo tunasherekea mpango huu unaolenga kubadilisha maisha. Kama wengi wenu mvyojua, upatikanaji wa nishati safi na salama ni msingi wa maendeleo, elimu, afya, pamoja na kuchangia ubora wa maisha kwa ujumla,”alisema.

Alisisitiza kwamba kampuni hiyo imeamua kufungua maduka hayo maeneo ya Temeke, Buguruni na Mwenge katika harakati za kuwaletea karibu wakazi wa jijini Dar es Salaam huduma za Sun king katika maeneo yao na kurahisisha biashara zao za kila siku na shughuli zao za nyumbani yakiongeea mtandao wa maduka yake mkoani Dar es Salaam yaliyopo maeneo mbalimbali ikiwemo Bunju, Kigamboni, Gongo la Mboto, Mbagala, Chanika

“kifaa hiki cha kisasa cha kubadilisha mkondo wa umeme kinaweza kuwasha jokofu , komputa mpakato, taa , waya za ulinzi za umeme na vifaa matumizi vingine kwa gharama na nafuu  na mteja anaweza kununua kwa njia ya mkopo na kulipa kidogo kidogo,” aliongeza msanii huyo Mpoto ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Bw. Mpoto alisema kwamba hivi karibuni kule Arusha kampuni hiyo ilifunguka mtambo wa kisasa kwenye hospitali ya jijni humo ili kusaidia wakinamama wakati wa kujifungua pindi umeme unapokatika na kupunguza atha ya mgao wa umeme.

Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Albert Msengezi alisema kwamba kampuni hiyo kwa sasa imesambaa nchini nzima na wanazidi kwenda vijini katika juhudi za kuwaletea watanzania mapinduzi ya umeme jua kwa kutumia nishati safi na kutunza mazingira.

“Leo tumezindua maduka yetu matatu hapa Dar es Salaam lakini tuna mengine maeneo ya chanika , vikindu na sehemu za pwani katika juhudi za kuleta suluhishi za nishati ya jua zinazopatikana kwa bei nafuu na kuchochea biashara endelevu na uchumi wa nchini, alisema Bw Msengezi

 

Pamoja na mambo mengine , Bw Msengezi alisema kwamba kifaa hiki kipya kinapanua huduma za Sun king kwenye mkondo wa waya za umeme jua na ikikamilisha na safu ya nguvu ya kituo cha umeme jua yenye nguvu nyingi  kuongeza waya ambayo upo kwenye mkondo wa kifaa cha kubadilisha mkondo wa umeme za Sun King.

“ikikamilisha safu ya kifaa cha kisasa chenye nguvu , ambayo ina uwezo wa kutoa kutoka 3.3 kVA hadi 20 kVA AC. Kifaa hiki kimeundwa kwa mahitaji makubwa zaidi, kutoka nyumbani na biashara hadi shule na vituo vya afya, ikitoa uhuru kamili wa nishati na suluhisho zinazoweza kubadilishwa,” alifafanua.

Aliongeza kwamba maduka haya mapya ni viashiria vya hatua muhimu katika dhamira ya kampuni hiyo ya kuwawezesha wananchi na jamii kupitia suluhisho za nishati endelevu huku ukionyesha ubunifu mpya wa kampuni katika teknolojia ya jua.

Kwa upande wake Bw Seth Mathemu, Meneja Mwandamizi Masoko alisema kwamba uzinduzi wa  kifaa hicho (Solar Energy Inverter)  ilikuwa ni ahadi ya kampuni hiyo kutoa suluhisho za nishati zinazoweza kuaminika na za bei nafuu kwenye ngazi ya familia na biashara kwa watanzania.

“Kifaa hiki kipya cha kisasa ni suluhisho kwa matumizi ya majokofu , televisheni na biashara ndogo ndogo , na mfumo huu una uwezo hadi 600W ya nguvu ya AC na kufanya kuwa suluhisho bora kwa kaya na biashara zinazokumba na changamoto ya kukatika kwa umeme kwenye hapa nchini,” alisisitiza

Naye Bw Aidan Byarufu ambaye ni Meneja wa Biashara wa kanda wa Soko la Mwenge , alisema kwamba kampuni hiyo ya kimataifa ina uzoefu wa muda mrefu kwenye nishati wa umeme jua kwa hiyo ni wakati muafaka kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuchangamkia fursa hiyo,

Kampuni hiyo ilisema pia kwa pamoja vifaa hivi vyenye nguvu zinapatikana kupitia mpango wa kifedha wa Sun King wa malipo kadri unavyotumia wa kulipa taratibu (EasyBuy), unaowezesha wateja kulipa kwa awamu  na kwa unafuu. Mifumo hii inatoa akiba kubwa katika gharama za mafuta ya jenereta na matengenezo, na haraka kujilipa  yenyewe.

Sun King ni kampuni inayoongoza duniani katika nishati ya jua isiyo kwenye gridi ya umeme, ikiwa na muundo wa kisasa wa bidhaa, ufadhili wa bei nafuu, na mfano wa usakinishaji wa jamii uliojengwa kutoa nishati kwa familia na biashara zinazoishi barani Afrika na Asia ambazo hazina ufikiaji wa umeme wa kuaminika. Ilianzishwa mwaka 2007, Sun King imeweka viwango vya dhahabu kwa utendaji wa nishati ya jua isiyo kwenye gridi na muundo kama sehemu ya dhamira yake: kuwezesha ufikiaji wa maisha bora.Meneja wa Kanda wa Soko la Mwenge, Aidan Byarufu akizungumza na wageni waalikwa, mawakala katika sherehe za uzinduzi wa Duka la Sun King Mwenge , mwishoni mwa wiki

Balozi wa Sun king na msanii maarufu Mrisho Mpoto akiwa na mawakala wa kampuni baada ya kufungua duka la Buguruni
Mrisho Mpoto , Balozi wa kampuni ya Sun king akionyesha moja ya vifaa vya umeme jua , baada ya uzinduzi wa duka hilo mwenge jijini Dar es Salaam.
Msanii Mrisho Mpoto akizungumza na waandishi wa habari , wageni waalikwa na mawakala kwenye uzinduzi wa duka la Mwenge, kulia kwake ni Meneja Mauzo wa Kampuni hiyo, Bw Albert Msengezi na kushoto ni Meneja Masoko Mwandamizi, Seth Mathemu , na mwisho kulia ni Meneja Biashara wa kanda, Aidan Byarufu wa Soko la Mwenge , kwenye uzinduzi rasmi wa duka la kampuni ya Sun kings yenye vifaa na mitambo ambayo ni suluhisho kwa umeme wa Jua.
Balozi wa Sun king, Mrisho Mpoto akizungumza na waandishi wa habari , pembeni yake ni Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Sun King, Albert Msengezi.
 

No comments