Header Ads

test

WAZIRI MHAGAMA AMPONGEZA DK.RAIS SAMIA,UINGEREZA KUTOKOMEZA MAGONJWA YASIYOPEWA KIPAUMBELE

 

Na Mwandishi Wetu


WAZIRI wa Afya Jenista Mhagama amesema anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali ya Uingereza kwa kuamua kufanya kazi ya kutokomeza magonjwa haya amabyohayapewi kipaumbele.

Ametoa shukrani hizo  Septemba 18, 2024 wakati wakiwa katika ziara pamoja na Princess Sophie (Duchess of Edinburgh) ambae ni Mke wa Mtoto wa Mfalme wa Uingereza walipotembelea Kituo Cha Afya cha Mlandizi mkoani Pwani kwa lengo la kujionea utoaji huduma za matibabu ya macho

"Yapo magonjwa ambayo hayajapewa kipaumbele sio Tanzania tu bali
Duniani kote ikiwemo ugonjwa huu wa macho ( Trakoma) lakini pia magonjwa kama mabusha, matende, minyoo ya tumbo, kichocho."

Aidha ametoa ra kwa Watanzania hasa wa Mkoa wa Pwani kushirikiana na Serikali kumhamasisha mwananchi yeyote mwenye dalili za ugonjwa wa macho kwenda
hospitali kwani ugonjwa huo husababisha upofu.

Kwa upande wake, Princess Sophie (Duchess of Edinburgh)  amesema lengo la Uingereza ni kuhakikisha Tanzania inatokomeza magonjwa yasiyopewa Kipaumbele.
"Haya yote yanawezekana kupitia ushirikiano ambao tunautoa kwa Tanzania ikiwa ni kwa mtu mmoja mmoja katika kutokomeza magonjwa ya trakoma,"amesema Sophie na kusisitiza kwa pamoja wanaweza kutokomeza ugonjwa huo wa
trakoma.
Ziara hiyo imemalizika kwa kumtembelea nyumbani kwake mnufaika
wa matibabu ya ugonjwa wa trakoma yanayotolewa na Serikali kupitia
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau akiwemo Sightsavers.












 

No comments