Header Ads

test

MWENYEKITI KIBUGUMO ,KIGAMBONI AJIVUNIA MAFANIKIO YAKE YA UONGOZI NDANI YA MIAKA MITANO

 

Na Mwandishi Wetu,DmNews tz online 


MWENYEKITI wa Serikali ya mtaa wa Kibugumo katika Halmashauri ya Wilaya Kigamboni Yusuph  Selemani Tindwa  Amesema kuwa katika kipindi cha uongozi wake amejitahidi kutatua Kwa kiwango kikubwa kero ya migogoro ya ardhi.

Amesema wakati anaingia madarakani  mwaka 2019 mtaa wa kibugumo ulikuwa na changamoto kubwa ya ardhi lakini baada ya kuchaguliwa Yeye na wajumbe wake Kwa kushirikiana na mamlaka zingine ilikuwa ni kutatua migogoro hiyo.

Mwenyekiti Tindwa  ameyasema hayo Leo Septemba 2, 2024 ofisni kwake  mtaani humo wakati  wa mahojiano maalumu na  DmNews tz online .ambapo amesema Kwa kazi kubwa ambayo amefanya wananchi wa mtaa huo hasa wazee wanatamani kuona anaendelea kuwa kiongozi wa mtaa huo miaka mingine mitano.

Amesema licha ya changamoto hizo za ardhi lakini amefanikiwa kuimarisha eneo la elimu Kwa kujenga shule katika mitaa wake ,kuimarisha eneo la afya ,miundombinu ya barabara pamoja na Kuchangia ujenzi wa ofisi za Chama kwenye mtaa wa kibugumo na kidete.
Wakati huo huo Mwenyekiti  Tindwa   amezungumzia utendaji kazi wa Rais .Dkt Samia Suluhu Hassan kwamba anafanya kazi yake ipasavyo na ndio maana wapinzani wanazidi kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM ) ili kuunga juhudi za kiongozi huyo mkuu wa nchi.










 

No comments