Header Ads

test

AGRISPARK YABAINI ASILIMIA 70 YA TAFITI NA VUMBUZI HAZIWASHIIKISHI WAKULIMA TOKA MWANZO.

Na: Calvin Gwabara – Morogoro.


Utafiti wa awali uliofanywa kuangalia mbinu za ushirikishi za watafiti na wakulima katika uvumbuzi na uhaulishaji wa Maarifa na teknolojia za kilimo umebaini kuwa zaidi ya asilimia 70 ya wakulima hawawashirikishwi katika hatua za awali za ubunifu na tekinolojia na kuchangia kuwa na mapokeo hafifu miongozi mwa wakulima na kutofanya vizuri kwa maarifa hayo.

Hayo yamebainishwa na Mtafiti mkuu mwenza wa Mradi wa Mbinu shirikishi za wanafunzi na wakulima katika uvumbuzi na uhaulishaji wa maarifa na teknolojia za kilimo (AGRISPARK) Dkt. Nicholaus Mwalukasa wakati akiwasilisha matokeo hayo ya awali ya mradi huo uliofanyika kwenye Wilaya ya Morogoro Manipsaa, Halamashauri ya Mvomero na Halmashauri ya Morogoro Mkoani Morogoro.

“Matokeo yetu yamebaini kuwa wakulima wengi wakulima walio wengi wanashirikishwa wakati tutafiti au teknolojia imeshakamilika wao wamekuwa wanashilikiswa zaidi kufanya majaribio pia kuona kama inafanya kazi kitu ambacho kinapelekea wakulima wengi kutokuwa na maarifa ya kutosha na uelewa na hivyo kuwa na mapokeo hafifu ambayo hayaleti tija iliyokusudiwa”Alieleza Dkt. Mwalukasa.

Aliongeza “Katika utafiti huu ulihusisha wakulima ambao wamewahi kushiriki katika ubunifu, technolojia au mradi wowote ambao ulifanywa na watafiti wa kutoka SUA, na hapa tulihusisha wakulima mbao wapo kwenye miradi au utafiti unaofanyika sasa au ule ambao ulishafanyika”.

Dkt. Mwalukasa amesema matokeo haya yanaamaanisha kwamba watafiti wanahitaji kuwashirikisha wakulima zaidi katika hatua za awali za uundaji wa maarifa na maendeleo ya ubunifu ili kuhakikisha teknolojia za kilimo zinafaa zaidi, zinapokelewa kwa urahisi, na kuwa endevu.

Pia amebainisha kuwa ni vyema watafiti wakashirikiana kwa karibu na Maafisa Ugani na Vikundi vya Wakulima ili kuimarisha usambazaji na upokeaji wa uvumbuzi wa kilimo, kwani makundi hayo yana ushawishi mkubwa katika kuwafikia na kuwaelimisha wakulima kwa ufanisi.

Akifungua warsha hiyo na uzinduzi wa mradi huo wa AGRISPARK, Rasi wa ndaki ya sayansi asilia na Tumizi (CoNAs) Dkt. Geofrey Karugila kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda amesema mradi huo ni matokeo ya maono makubwa ya Chuo katika kuinua watafiti wake hasa wachanga kwa kutenge fedha za ndani ili wafanye tafiti za kusaidia kutatua changamoto za jamii na taifa.

“Zipo tafiti nyingi ambazo zinafanywa na watafiti wa SUA kwakuwa kila mwaka Chuo hutenga kiasi cha shilingi Bilioni moja kusaidia kufanya tafiti hizo na mradi huu wa AGRISPARK ni sehemu ya matunda ya fedha hizo za serikali ambazo zinasaidia kuleta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabiliwa watanzania huku zikiwajengea uwezo watafiti wetu hapa chuoni” Alisema Prof. Karugila.

Dkt. Karugila amewataka watafiti kushirikiana na jamii katika kubuni mbinu ambazo zinaweza kusaidia kuondoa changamoto zao ili jamii iweze kunufaika na kazi kubwa zinazofanywa nao badala ya kutumia fedha na rasilimali zingine na kuzalisha bunifu ambayo haitatumiwa na jamii.

Nae kwa upande wake mtafiti mkuu wa mradi huo wa AGRISPARK Dkt. Philbert Nyinondi kutoka SUA amesema mradi huu umekuwa wa kipekee kwakuwa si tu kwakuwa unafadhiliwa na fedha za ndani bali unajibu moja kwa moja changamoto zinazoikabili jamii.

“Mara nyingi tunapokuwa tunafanya tafiti ambazo tumefadhiliwa na wafadhili toka nje ya nchi unapewa fedha kulingana na ajenda ya mtoa fedha au kitu anachokipenda lakini tafiti zilizofadhiliwa na fedha zetu wenyewe moja kwa moja huwa inakwenda kugusa maisha ya watu kwa maana tunafanyia utafiti kitu au jambo ambalo moja kwa moja tunataka kama taifa kwa maendeleo yetu” alifafanua Dkt. Nyinondi.

Mtafiti huyo mkuu wa mradi amesema jambo lingine kubwa ambalo mradi unafanya ni kuwashirikisha zaidi wanafunzi kwenye utafiti huo ili kuwafanya wanapomaliza wewe wanajua changamoto zinazowakabili wakulima kuanzia wanapoandaa shamba hadi kuvuna na kufikiria mbinu za kuzitatua badala ya kwenda na taaluma na mbinu ambazo haziwezi kusaidia jamii kwenye mazingira fulani.

“Kwahiyo tunakwenda sambamba wote kwa pamoja, wakulima,wanafunzi na watafiti kuanzia hizi hatua za awali kabisa hadi mwisho hatua kwa hatua ili maarifa tutakayozalisha,ubunifu tutakaoupata yawe ni matokeo yetu wote maana sina haja tena ya kwenda kumfundisha mkulima maana alikuwa ni sehemu ya umchakato hivyo kwa njia hii tutakuwa na matokeo endelevu kwa wakati wote” alieleza Dkt. Nyinondi.

Amesema mradi huo unalenga kuangalia namna ambavyo jamii ya wananchi wanaozunguka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo inavyoweza kunufaika na uwepo wa chuo hicho lakini matokeo yake ndiyo yatapelekea mradi kutoka usambazwe nje ya Mkoa wa Morogoro au la.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa utafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH Bi. Hildegalda Mushi amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na watafiti wa Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo katika kutatua changamoto zinawazowakabili wakulima na taifa kwenye sekta ya kilimo.

Amesema COSTECH kama Taasisi inayosimamia tafiti na kutoa ushauri kwa serikali kwenye masuala mbalimbali ya Kisayansi, teknolojia na ubunifu nchini itaendelea kushirikia na watafiti wote nchini na kuunga mkono juhudu zao mbalimbali kwa kuwawezesha kupata fedha za kufanya tafiti hizo ili sisaidie kuwakomboa watanzania.
Mtafiti mkuu mwenza wa Mradi wa Mbinu shirikishi za wanafunzi na wakulima katika uvumbuzi na uhaulishaji wa maarifa na teknolojia za kilimo (AGRISPARK) Dkt. Nicholaus Mwalukasa akiwasilisha matokeo ya awali.Rasi wa Ndaki ya Sayansi asilia na Tumizi (CoNAs) Dkt. Geofrey Karugila akifungua warsha hiyo kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda.Mtafiti mkuu wa mradi huo wa AGRISPARK Dkt. Philbert Nyinondi kutoka SUA akieleza upekee wa mradi huo.Mkurugenzi wa utafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH Bi. Hildegalda Mushi akitoa salamu za COSTECH.Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi.Dkt. Beatrice Lyimo kutoa COSTECH akiwasilisha mada yake kuhusu Ubunifu wa Kilimo na Bioteknolojia ya kisasa kwa wadau hao.Rasi wa Ndaki ya Sayansi asilia na Tumizi (CoNAs) Dkt. Geofrey Karugila akifungua warsha hiyo kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda akibonyeza kitufe kuzindua mradi huo.Mkuu wa Idara ya Infomatiki na teknolojia ya habari na mawasiliano Dkt. Michael Mahenge akitoa neno la idara kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua warsha hiyo.






No comments