Header Ads

test

MHE. KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA KAMPASI YA TANGA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete, ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Tanga, leo tarehe 20 Februari 2026. 

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mheshimiwa Kikwete amethibitisha kuwa serikali imeamua kutumia kiasi cha shilingi bilioni 39 kwa ajili ya ujenzi wa kampasi hiyo, fedha zitakazotengwa kila mwaka hadi kukamilika kwa mradi mzima.
 
 “Namshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samaia Suluhu Hassan kwa kukubali na kuruhusu kutenga kiasi cha shilingi Bill 39 za ujenzi wa Kampasi ya Tanga” amesema Mhe. Kikwete. 
Aidha, amesisitiza ujenzi wa mradi wa kampasi ya Tanga unatokana na elimu kuwa kipaumbele na kusisitiza kuwa serikali   itaendelea kuwekeza katika elimu na kuhakikisha utumishi wa umma unaboreshwa nchini ambalo ni jukumu la chuo kuwajengea uwezo watumishi wa umma nchini.

Pia Mhe. Kikwete amesema kuwa, ameridhishwa na kiwango cha kazi kilichofanyika na kuipongeza menejimenti ya chuo kwa kusimamia kwa makini ujenzi wa kampasi. Amesema kuwa ujenzi huu unalenga kuimarisha huduma za utumishi wa umma nchini kupitia kampasi itakayojenga mustakabali mzuri wa elimu na utumishi bora.

    Akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi, Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho amesema kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi ilianza rasmi tarehe 8 Februari 2025, ikiwa ni ujenzi wa jengo la ghorofa mbili la  madarasa gharama za takriban shilingi bilioni 6.16. 

Dkt. Mabonesho amesema kua, Jengo litajumuisha madarasa 26 yatakayohudumia zaidi ya wanafunzi 2,500 kwa awamu moja, ofisi 24 za watumishi, kumbi mbili za mikutano, na vyoo vya kisasa 18. Vilevile, amesema jengo hili litakuwa na miundombinu ya kisasa ya TEHAMA itakayowezesha matumizi ya teknolojia katika kufundisha, kujifunza, na kuendesha shughuli za kitaaluma kwa ufanisi zaidi.

Dkt. Mabonesho pia alibainisha kuwa mradi huu utaleta manufaa makubwa kwa wananchi kiuchumi kutokana na huduma zitakazotolewa na chuo, ikiwemo kuimarisha ajira na maendeleo ya kijamii. Ujenzi huu unaonyesha dhamira ya serikali ya kuimarisha sekta ya elimu na utumishi wa umma nchini, na kuleta maendeleo zaidi kwa mkoa wa Tanga na taifa kwa ujumla.

Mradi wa ujenzi wa Kaampasi ya Tanga unatekelezwa katika eneo la hekari 14 lililopo Kange Uzunguni, mjini Tanga. Awamu ya kwanza ya ujenzi ilianza rasmi tarehe 8 Februari 2025,













 

No comments