Header Ads

test

FURAHA YATANDA KWA KINAMAMA WA JAI BAADA YA RAMADHANI CHARITY PROGRAM KUTOA IFTAR

Furaha imetanda kwa kinamama wa taasisi ya JAI baada ya kupokea sadaka ya Iftar kutoka kwa taasisi ya Ramadhani Charity Program 2026, ikiwa ni sehemu ya kuendelea kusaidia jamii katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Akizungumza wakati wa kukabidhi sadaka hiyo, Mwenyekiti wa Ramadhani Charity Program 2026, Ahmed Misanga, aliwapongeza kinamama wa JAI kwa kuwa mstari wa mbele katika kujitolea na kusaidia jamii.

Misanga alisema kuwa JAI ni washirika wa karibu wa Ramadhani Charity Program, hivyo wameona ni vyema kufika na kuwapatia sadaka ya Iftar kama ishara ya kutambua mchango wao mkubwa katika kusaidia jamii.

Aidha, alitumia fursa hiyo kumuombea dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na viongozi wengine wa nchi ili waendelee kuiongoza Tanzania kwa amani, umoja na mafanikio.

Kwa upande wake, Kiongozi wa JAI Mkoa, Bi. Aisha Ramadhani, alisema tukio hilo ni faraja kubwa kwao kwani linaonyesha kuwa kazi wanazozifanya za kujitolea zinatambuliwa na kuthaminiwa.

Alimshukuru Ahmed Misanga na Ramadhani Charity Program kwa kuwapatia sadaka hiyo, akisema Allah atawalipa kwa wema huo na wao wataendelea kuwaombea dua kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kusaidia watu wenye uhitaji katika jamii.

Katika hafla hiyo, kinamama wa JAI walipokea msaada wa vyakula vikiwemo tambo, ngano na tende, pamoja na fedha kwa ajili ya mboga kwa ajili ya Iftar.



 

No comments