PROMOSHENI YA “SHINDA BODA” YAMPA PIKIPIKI MKAZI WA DAR, ASEMA NI FURSA YA AJIRA KWA VIJANA
Na Mwandishi Wetu
Ndoto ya kujikwamua kiuchumi kwa vijana wengi imepata mwanga mpya baada ya mkazi wa Dar es Salaam, Jerome Mushi, kujishindia pikipiki aina ya TVS kupitia promosheni ya “Shinda Boda” inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya PigaBet Tanzania.
Mushi alisema ushindi huo ni fursa muhimu kwake na kwa kijana mwenzake kwani anapanga kuitumia pikipiki hiyo kuanzisha shughuli ya usafirishaji wa bodaboda ili kujiongezea kipato na pia kutoa ajira kwa kijana mwingine.
“Vijana wengi tunapambana mtaani ili kujikwamua kiuchumi, nami ni mmoja wao waliobahatika. Namshukuru Mungu kwa ushindi huu kwani utanisaidia pia kumfungulia fursa kijana mwenzangu aingie mtaani kufanya biashara ya bodaboda,” alisema Mushi.
Aliongeza kuwa amekuwa akishiriki mara kwa mara katika michezo hiyo na kupata ushindi mdogo mdogo, lakini safari hii amepata ushindi mkubwa ambao anaamini utabadilisha maisha yake.
Kwa upande wake, Afisa Masoko wa PigaBet Tanzania, Hemed Msonge, alisema promosheni ya “Shinda Boda” imeanzishwa kwa lengo la kuwainua Watanzania kiuchumi kwa kuwapatia zawadi za pikipiki.
Alisema katika promosheni hiyo kampuni hiyo inatoa pikipiki mbili kila wiki kwa kipindi cha wiki sita mfululizo kwa washindi wanaoshiriki katika michezo yake.
Msonge aliwahimiza Watanzania kushiriki katika promosheni hiyo kwa uwajibikaji, akibainisha kuwa droo zitaendelea kufanyika kila wiki hadi mwisho wa kampeni.
“Tunawaalika Watanzania wengi kushiriki katika promosheni hii kwa uwajibikaji. Kaulimbiu yetu ni Cheza, shinda boda na ubadilishe maisha yako,” alisema Msonge.
.jpeg)

.jpeg)
Post a Comment