Header Ads

test

SENEGAL YAVULIWA UBINGWA AFCON 2025, MOROCCO YATANGAZWA MSHINDI

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

SHIRIKISHO la Mpira Barani Afrika kupitia bodi ya (CAF,) imeamua kwamba Senegal wamefanikiwa "kujitoa mchezoni" (forfeit) na hivyo Morocco kutangazwa washindi wa michuano kwa ushindi wa 3-0 kwa mujibu wa sheria za mashindano.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CAF na kuzua mijadala imeeleza kuwa Senegal walikiuka Kifungu cha 82 cha kanuni za mashindano hayo ya kuwania Kombe la Mataifa  Barani Afrika, na hivyo Kifungu cha 84 kikatumika.

Kifungu cha 82 kinasema kuwa ikiwa timu itakataa kucheza au itaondoka uwanjani kabla ya kumalizika kwa muda wa kawaida bila idhini ya mwamuzi, itachukuliwa kuwa imeshindwa na kuondolewa kwenye michuano, huku

Kifungu cha 84 kikikazia masharti hayo kuwa timu yoyote itakayokiuka Kifungu cha 82 itaondolewa kabisa na kupoteza mechi kwa 3-0.

Kutangazwa kwa ushindi huo kwa Morocco dhidi ya Senegal kumetokana na kitendo cha timu ya Senegal kutoka uwanjani kabla ya mechi kumalizika ambapo Senegal waliilaza Morocco kwa bao 1-0 katika fainali iliyochezwa tarehe 18 Januari.

 Fainali hiyo iligubikwa na utata baada ya  wachezaji wa Senegal kukataa kuendelea na mchezo baada ya wenyeji (Morocco) kupewa penati katika dakika za nyongeza wakati mechi ilikuwa bado 0-0.

Baada ya kuchelewa kwa takribani dakika 17, wachezaji walirudi uwanjani ambapo Brahim Diaz ilikosa mkwaju wa penati katika dakika ya 114 kabla Pape Gueye wa Senegal kufunga bao pekee la ushindi katika dakika ya 107.

No comments