Header Ads

test

WAKAZI 600 DAR WAPEWA SIKU 14 KULIPA MADENI PANGO LA ARIDHI


WAKAZI zaidi ya 600 wa Dar es Salaam wamepewa siku 14 kulipa madeni ya pango la ardhi ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria.Kamishna Msaidizi wa Wizara ya Ardhi Mkoa huo, Shukrani Kyando, amesema hayo leo Aprili 24,2026  ambapo amesema kuwa wadaiwa hao tayari waliwahi kupewa notisi ya zaidi ya miezi mitatu pamoja na kukumbushwa mara kadhaa bila mafanikio.

“Kabla ya kufikia hatua ya kuwafikisha mahakamani, wizara imefuata taratibu zote za kibusara kwa kuwapa wadaiwa muda wa siku 14, siku 90, na sasa imeongeza tena siku 14 kuanzia Aprili 24, 2026.”

Kwa mujibu wa Kyando, yeyote atakayeshindwa kulipa ndani ya muda huo atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka kwa mujibu wa sheria.
Amesisitiza kila mmiliki wa ardhi ana wajibu wa kulipa pango la ardhi kwa wakati, na kushindwa kufanya hivyo kunaweza kusababisha kupoteza haki ya umiliki pamoja na kukosa sifa za kupata mikopo.

“Mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa na lengo la kukusanya shilingi bilioni 83, lakini hadi sasa zimekusanywa takribani shilingi bilioni 63, hali inayochelewesha kufikiwa kwa malengo ya asilimia 100.”
Kwa upande wake, Mratibu wa Kodi Mkoa huo, Alfred Thomas, amewataka wananchi kulipa kodi kwa wakati ili kulinda haki zao za msingi katika umiliki wa ardhi.


 

No comments