ZIARA YA KAMATI YA UTEKELEZAJI YA JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA DAR ES SALAAM – JIMBO LA KIBAMBA
Leo tumefungua rasmi ziara ya Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanza katika Jimbo la Kibamba.
Akizungumza na viongozi wa Kata na Matawi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam, Khadija Ally, amewashukuru kwa moyo wa kujitolea, uzalendo, mshikamano na ushiriki wao wa hali na mali katika kufanikisha shughuli za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
“Uzalendo wenu, mshikamano wenu, kujitolea kwenu na imani yenu kwa Chama Cha Mapinduzi vimechangia kwa kiwango kikubwa mafanikio ya chama na ushindi uliopatikana.”
Ziara hii inalenga kuwashukuru viongozi na wanachama wetu, kuimarisha umoja na mshikamano, pamoja na kuhamasisha ari ya utendaji kazi katika kuendelea kuijenga Jumuiya ya Wazazi na Chama Cha Mapinduzi kwa maendeleo ya Taifa letu.
Katika ziara hii, Kamati ya Utekelezaji ya Mkoa wa Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake Khadija Ally itatembelea Kata zote 102 za Mkoa wa Dar es Salaam na kugawa tuzo za pongezi na shukrani kwa viongozi wa Kata kwa mchango wao mkubwa katika kuimarisha chama.Tunawathamini, tunawapenda, na tunaamini kuwa nguvu ya Chama Cha Mapinduzi ipo kwa wanachama wake wenye uzalendo, uaminifu, mshikamano na imani thabiti kwa chama chao.
#JumuiyaYaWazaziDSM
#UmojaMshikamanoNaMaendeleo
#CCMKaziIendelee
#ZiaraYaShukrani2026

.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
Post a Comment