Header Ads

test

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA DKT. GRACE MAGEMBE, KAMISHNA WA DCEA ARETUS LYMO WATEMBELEA BANDA LA TMDA SABASABA 2026

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, ametembelea banda la TMDA katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) na kupongeza juhudi za Mamlaka katika kudhibiti bidhaa duni na bandia za afya.

Aidha, ameitaka TMDA kuendelea kuimarisha elimu kwa umma kuhusu matumizi salama ya bidhaa za afya ili kulinda afya ya wananchi.

"Tumieni watoa huduma wa ngazi ya Jamii kusaidia kufikisha elimu matumizi salama ya bidhaa za afya kulinda Wananchi.

TMDA mnafanya kazi nzuri na hongereni sana." Amesema Dkt. Grace Magembe.

Mbali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, pia TMDA ilipata mgeni Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Ku

pambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Bw. Aretus Lymo na kuipongeza Mamlaka kwa kazi kubwa ya udhibiti wa bidhaa za afya inayolenga kulinda afya ya wananchi.

Maonesho hayo ya Kimataifa Sabababa yanaendelea hadi Julai 13, 2026.

TMDA ipo kwenye maonesho hayo kutoa elimu kwa Jamii hususani bidhaa duni na bandia na matumizi sahihi ya Dawa.Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akipokea nakala ya toleo la miaka 20 ya TMDAKatibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akipata maelezo kuhusu Mahabara inayohamishika (Min kit lab) ambayo ipo katika banda hilo la TMDA ndani ya SabasabaKamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Bw. Aretus Lymo  (kulia) akipata maelezo kuhusu shughuli za TMDA kutoka kwa Gaudensia Siimwanza Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma.

 

No comments