PPAA YASHUGHULIKIA RUFAA 58 KWA MWAKA FEDHA 2025/26
Mkuu wa Sehemu ya Sheria wa PPAA, Bi. Agnes Sayi akizungumza na waandishi wa Habari kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando katika banda la PPAA lililopo ndani ya banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam
Yaiwezesha Serikali kupata thamani halisi ya fedha
Wadau ununuzi wa umma 2,600 wafikiwa mafunzo matumizi ya moduli
Na Mwandishi wetu
MAMLAKA ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imefanikiwa kushughulikia rufaa 58 kati ya rufaa 60 zilizowasilishwa katika mwaka wa fedha 2025/26 na kuzitolea uamuzi kwa wakati na kuiwezesha Serikali kupata thamani halisi ya Fedha.
Takwimu hizo zimetolewa na Mkuu wa Sehemu ya Sheria wa PPAA, Bi. Agnes Sayi kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando katika banda la PPAA lililopo ndani ya banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
“Katika mwaka wa fedha 2025/26 PPAA ilipokea rufaa takriban 60 na kushughulikia rufaa 58 kati ya 60 zilizowasilishwa na kuzitolea uamuzi kwa wakati, rufaa mbili zilizosalia zimefanyiwa kazi katika mwaka huu wa fedha,” amesema Bi. Sayi
Aidha, Bi. Sayi ameongeza kuwa baada ya Serikali kuweka sharti la lazima kuwa ununuzi wa Umma kufanyika kwa njia ya Kieletroniki, PPAA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) ilijenga Moduli ya Kupokea na Kushughulikia Malalamiko na Rufaa katika Mfumo wa NeST, na moduli hiyo imeanza kutumika tangu mwezi Februari 2025.
“Ili kuwawezesha wadau wa Ununuzi wa Umma kutumia Moduli hiyo, PPAA imefanikiwa kutoa mafunzo ya matumizi ya Moduli ya Kupokea na Kushughulikia Malalamiko na Rufaa katika mfumo wa NeST kwa wadau wa ununuzi wa umma 2,600 nchini,” amesema Bi. Sayi na kuongeza kuwa mafunzo hayo yaliwahusisha wazabuni takriban 1,907 pamoja na watumishi wa umma 705.
Bi. Sayi ameongeza kuwa PPAA katika maonesho ya Sabasaba inatoa elimu juu ya uwasilishaji na ushughulikiaji wa malalamiko na rufaa zinazotokana na mchakato wa ununuzi wa umma, juu ya rufaa zinazotokana na kufungiwa kushiriki katika michakato ya ununuzi wa umma pamoja na juu ya malalamiko yanayotokana na kushindwa kwa Afisa Masuuli kutoa uamuzi ndani ya muda uliowekwa.
Maeneo mengine yanayotolewa elimu ni kuhusu malalamiko baada ya mkataba wa ununuzi kuanza kutekelezwa, uamuzi juu ya maombi ya kuongezewa muda wa kuwasilisha rufaa nje ya muda uliowekwa, uamuzi juu ya maombi ya utekelezaji wa amri ya Mamlaka ya Rufani, uamuzi juu ya maombi ya kufuta uamuzi uliotolewa bila kusikiliza upande mwingine na uamuzi juu ya maombi ya kurejesha rufaa.
Maonesho ya Sabasaba kwa mwaka 2026 yanaongozwa na kaulimbiu: Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania.

Post a Comment