Header Ads

test

TUMAINI JIPYA:WATOTO SABA WAFUNGULIWA DUNIA YA USIKIVU MUHIMBILI.

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo, Julai 27, imewasha vifaa vya usikivu (Cochlear Implant) kwa watoto saba waliopandikizwa vifaa hivyo, ikiwa ni mwendelezo wa huduma za kibobezi za upandikizaji huo zilizozinduliwa rasmi mwaka 2017 ambapo hadi sasa hospitali imefanikiwa kuwafanyia upasuaji wa kupandikiza vifaa vya usikivu wagonjwa 115 na kuwa hospitali ya kwanza barani Afrika.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Bw. Emmanuel Tayari, amepongeza hatua hiyo na kubainisha kuwa serikali inaendelea kuweka mikakati thabiti ya kusogeza huduma za kibobezi karibu na jamii ili kuliokoa Taifa dhidi ya changamoto za kiafya zinazoweza kuepukika.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Dkt. Dellilah Kimambo, ameeleza kuwa tangu mwaka 2017 Wizara ya Afya kupitia Muhimbili iliazimia kimkakati kuleta huduma za kibobezi nchini lengo ikiwa ni kuzuia wagonjwa kusafiri nje ya nchi na kupunguza gharama kubwa walizokuwa wakizibeba wananchi na kupunguza rufaa za matibabu nje ya nchi ambayo yalikua yanagharimu takribani shillingi mil 120 kwa mgonjwa mmoja ambapo kwa sasa hivi matibabu hayo yanatolewa hapa hapa Nchini kwa gaharama ya TZS. 45 Mil.

"Sasa hivi duniani inajulikana kwamba mtoto mwenye matatizo ya kusikia akipandikizwa kifaa hiki kwa wakati husika, ataweza kusikia kama kawaida na kuepuka changamoto za kuwa kiziwi tulipoamua kuleta huduma hii hapa nchini, wagonjwa wengi waliokuwa wakikosa huduma hapo awali sasa wamefaidika, na inawawezesha kuendelea na maisha yao ya kawaida,"  amesema Dkt. Kimambo.

Muhimbili inaendelea kuboresha huduma hii ambayo inatajwa kuwa unatajwa kuwa muhimu katika kuhakikisha watoto wanaozaliwa au kupata changamoto za usikivu wanapata fursa sawa ya kusoma na kushiriki katika ujenzi wa Taifa bila kikwazo cha ulemavu wa kutosikia.












 

No comments