RIDHIWANI: TANZANIA, UJERUMANI ZAZIDI KUIMARISHA USHIRIKIANO WA MAENDELEO
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani J. Kikwete, amesema uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Ujerumani umeendelea kudumu kwa muda mrefu na kujengwa katika misingi ya kuheshimiana, ushirikiano wa dhati na dhamira ya pamoja.Mhe. Ridhiwani ameyasema hayo Septemba 25, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Ujerumani, ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Amesema ushirikiano wa maendeleo ni sehemu muhimu ya mahusiano kati ya Tanzania na Ujerumani, ambapo taasisi za Ujerumani, ikiwemo GIZ na KfW Development Bank, zimeendelea kushiriki katika juhudi za kuchochea maendeleo ya Tanzania kupitia maeneo mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.
Aidha, Mhe. Ridhiwani amesema Tanzania inapitia mabadiliko makubwa ya kiuchumi yanayoongozwa na Dira ya Maendeleo 2050, ikiwemo utekelezaji wa ajenda ya viwanda yenye lengo la kujenga uchumi wenye ushindani, kuongeza uzalishaji na kukuza thamani ya bidhaa zinazozalishwa nchini.
Sambamba na hayo, amesisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na Ujerumani katika maeneo ya viwanda, uchakataji wa mazao, nishati, miundombinu, teknolojia na ukuzaji wa ujuzi, pamoja na sekta nyingine zenye uwezo wa kuongeza fursa za ajira na thamani katika mnyororo wa uzalishaji.


.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
Post a Comment