WAZIRI WA UWEKEZAJI ALIVYOSHANGAZWA NA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA SEKTA YA KILIMO SONGEA
Na Albano Midelo,Songea
uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo ambapo katika Halmashauri ya
Madaba na Songea mkoani Ruvuma wawekezaji toka nje wamewekeza
katika mashamba yenye ukubwa wa hekta zaidi ya 2500.
Akiwa katika Halmashauri ya Madaba,Waziri Mkumbo alishuhudia
uwekezaji mkubwa wa Kampuni ya kigeni ya Silver Ndolela iliyowekeza
katika shamba lenye ukubwa wa hekta 1500 ambapo kampuni hiyo
inazalisha mbegu za aina nne kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji.
Meneja wa shamba hilo alizitaja mbegu zinazozalishwa na Kampuni hiyo
kuwa ni maharagwe,mahindi,ngano na viazi ambapo Waziri Mkumbo
alisisitiza uwekezaji katika mbegu bora ni muhimu hapa nchini kwa kuwa
moja ya changamoto katika kilimo ni upatikanaji wa mbegu bora.
“Wakulima wetu wanatumia mbegu hafifu wanalima eneo kubwa na kupata
mavuno kidogo,hivyo uwepo wa shamba hili la mbegu bora itasaidia
kuboresha kilimo hapa nchini ’’,alisisitiza Waziri Mkumbo.
Waziri wa Mipango na Uwekezaji pia alikagua shamba kubwa la kilimo cha
umwagiliaji la Kampuni ya AVIV katika Kijiji cha Lipokela Halmashauri ya
Wilaya ya Songea.
Prof.Mkumbo amefurahishwa na uwekezaji mkubwa katika shamba
kahawa uliofanywa na Kampuni ya AVIV TANZANIA LTD ambapo Kampuni
hiyo inalima na kuchakata kahawa kwa mwaka tani zaidi ya 2000 katika
shamba la kahawa lenye ukubwa wa hekta zaidi ya 1000.
Waziri Mkumbo amesisitiza kuwa kulima na kuchakata kahawa ni
uwekezaji mkubwa ambao umefanywa kwa kuwezeshwa na Kituo cha
Uwekezaji nchini (TIC) ambapo amesema uwekezaji huo unashughulikia
sekta ya kilimo ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa.
Ameipongeza Kampuni ya AVIV kwa kutekeleza mambo matatu kwa wakati
mmoja ikiwemo kilimo cha kahawa,kuchakata mazao ya kilimo hivyo kutoa
ajira kwa watanzania na kuongeza mauzo nje ya nchi.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Kapenjama Ndile
akizungumza baada ya Waziri kutembelea maeneo ya uwekezaji katika
shamba la Madaba na Lipokela,ameutaja Mkoa wa Ruvuma kwa miaka 13
sasa unaongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula nchini.
Amesema katika kutambua mchango wa Mkoa wa Ruvuma kwenye
uzalishaji chakula ,mwaka huu kwenye maadhimisho ya Nanenane Kitaifa,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan
alitoa chetu maalum kwa Mkoa wa Ruvuma kwa kushika nafasi ya kwanza
kwa uzalishaji nafaka.
Awali akitoa taarifa ya Kampuni ya AVIV, Meneja Msaidizi wa Kampuni ya
AVIV TANZANIA Muthana Namb amesema asilimia 80 ya kahawa
inayochakatwa na Kampuni hiyo inauzwa katika nchi mbalimbali Duniani
zikiwemo Marekani,Saudi Arabia,India, Japan, Jordan na Afrika ya Kusini.
Naye Mwakilishi wa Kampuni hiyo anayesimamia kilimo Johson Kishumba
amesema Kampuni ya AVIV TANZANIA imekuwa kampuni ya kwanza
katika bara la Afrika kupewa Tuzo ya Water Stewardship inayotolewa na
SGS ya nchini Afrika ya Kusini kwa kufanya vizuri kwenye kilimo na
mazingira.
Hata hivyo amesema kampuni hiyo inashirikiana na wananchi
wanaozunguka shamba hilo ambao wamekuwa wanasaidiwa katika sekta
za afya,maji na mazingira na kwamba baadhi ya wananchi wanapata ajira
kwenye shamba la kahawa.
Waziri wa Mipango na Uwekezaji alifanya ziara ya kikazi ya siku mbili
mkoani Ruvuma kwa lengo la kukutana na wawekezaji,kusikiliza mafanikio
na changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi hatimaye kuimarisha zaidi eneo
la uwekezaji.
katikati ni Waziri wa Mipango na Uwekezaji Prof.Kitila Mkumbo akikagua uwekezaji uliofanywa na Kampuni ya SILVER NDOLEA katika uzaloshaji wa mbegu bora za mahindi,maharage,viazi na ngano katika shamba lenye ukubwa wa hekta 1500 katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea.
Waziri wa Mipango na Uwekezaji Prof.Kitila Mkumbo akizungumza baada ya kukagua uwekezaji uliofanywa na Kampuni ya AVIV TANZANIA katika sekta ya kilimo katika zao la kahawa lenye ukubwa wa hekta zaidi ya 1000 kwenye kijiji cha Lipokela Halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya AVIV TANZANIA Muthanna Namb akitoa taarifa ya utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa Waziri wa Mipango na Uwekezaji Prof.Kitila Mkumbo alipotembelea eneo la uwekezaji.Shamba la kahawa lenye ukubwa wa hekta 1000 katika kijiji cha Lipokela wilayani Songea ambapo Kampuni ya AVIV Tanzania inalima kahawa na kuchakata zao hilo ambapo kila mwaka tani 2000 za kahawa zinachakatwa na kuuzwa nchi mbalimbali duninai.
Post a Comment