Header Ads

test

ORYX GAS YAGAWA MITUNGI 700 NA MAJIKO YAKE WILAYANI IRAMBA

Na Mwandishi Wetu, Iramba

MKURUGENZI Mkuu wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman amesema uamuzi wa kampuni hiyo kugawa mitungi ya gesi 700 na majiko yake wilayani Iramba mkoani Singida unalenga kusogeza nishati safi ya kupikia karibu na wananchi.

Araman ameyasema hayo wilayani Iramba mkoani Singida wakati wa kukabidhi mitungi ya gesi na majiko yake kwa wananchi wakiwemo baba na mama lishe lengo likiwa kuwaunga mkono katika juhudi zao za kujiendeleza kiuchumi.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Seleman Mwenda akimwakilisha Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Fedha Dk.Mwigulu Nchemba.

“Oryx Gas tunaamini ukipika kwa kutumia gesi inaleta maendeleo mengi kwa jamii yetu. Pia kupika kwa gesi ya Oryx ni kulinda mazingira kwa kuacha kukata miti.Zaidi ya yote ni kulinda afya ya wanawake kwa kuwaepusha kuvuta moshi na mvuke unaoathiri mapafu na afya yao unaotokana na kuni na mkaa.”

Akieleza zaidi amesema kwa miaka mingi Oryx Gas imekuwa kampuni kinara katika kukuza matumizi ya gesi nchini na kuanzia mwaka Julai mwaka 2021 wamekuwa mstari wa mbele kutekeleza maelekezo ya Serikali ya kuhakikisha ifikapo 2032  asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia,” amesema.

Ameongeza Oryx Gas inatekeleza juhudi za Serikali za kueneza matumizi ya nishati safi kwa wananchi kwani hiyo ndio ndoto kubwa ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuona matumizi ya nishati safi ya kupikia yanapewa kipaumbele.

Pia, amemshukuru Dk. Nchemba kwa kuwa balozi mzuri wa kuleta maendeleo kwa wanawake na jamii kwa ujumla kwa kuiunga mkono Oryx Gas Tanzania katika mpango wa matumizi ya nishati safi mkoani  Singida.

 “Tunafurahi kumkabidhi mitungi ya gesi 700 kwa wakazi wa Iramba ambayo inathamani ya zaidi ya Sh.

milioni 50.Nawashukuru sana kwa nafasi hii mliyonipa,” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Seleman Mwenda amesema wamegawa mitungi hiyo kwa baba na mama lishe ikiwa ni sehemu kumuunga mkono Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuhimiza wananchi kutumia nishati safi ya kupikia.

Amesema kupika kwa gesi kunasaidia kutunza mazingira pamoja na afya hasa kwa wanaojihusisha  na shughuli za upishi huku akifafanua wamegundua misitu inateketea kwa sababu ya matumizi ya kupikia,”amesema.

Ameongeza athari nyingi ambazo wanazipata baba na mama lishe zinatokana na mkaa pamoja na kuni na hivyo kuathiri afya zao.“Katika kuunga mkono juhudi za Serikali tuliamua kuwasiliana na Oryx na tunashukuru wameitikia mwito.”
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Seleman Mwenda( wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania Benoite Araman(wa pili kulia) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya Oryx Ezekiel Daghora (katikati) ambaye ni Baba Lishe wakati wa tukio la ugawaji mitungi 700 kwa wananchi wa Wilaya ya Iramba wakiwemo wajasiriamal.






No comments