Header Ads

test

SHINDANO LA KCB EAST AFRICA GOLF TOUR KURINDIMA AGOST 03 LUGALO

 




SHINDANO la wazi la mchezo wa Gofu”KCB East Africa Golf Tour” linatarajiwa kufanyika Agosti 3 katika Klabu ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania-JWTZ Lugalo Gofu Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Leo Julai 24,2024 Mwenyekiti wa klabu ya Gofu Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amesema, shindano hilo la siku moja limelenga kupata wachezaji wanne watakaoiwakilisha nchi kwenye michuano ya Afrika Mashariki itakayofanyika Kenya.

Alisema shindano hilo litakuwa la ndani na kuhimiza wachezaji wa Gofu waliopo Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha ili kujaribu bahati yao.

“Hili litakuwa ni shindano la kipekee litakalodhaminiwa na KCB nchini Tanzania na watakwenda na nchi nyingine za Afrika Mashariki kufanya shindano kama hili na kutafuta wawakilishi watakaoenda fainali kule Kenya. Tunashukuru kwa kutudhamini,”amesema.

Aidha washindi wanne wa kila nchi watadhaminiwa kila kitu katika safari yao ya kuelekea kwenye fainali za Kenya.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa KCB Bank Tanzania Cosmos Kimario amesema shindano hilo litakuwa likifanyika kila mwaka huku lengo likiwa ni kuendeleza mchezo huo.

Nahodha wa Lugalo Gofu Japhet Masai amesema, Shindano hilo litachezwa kwa mfumo wa kimataifa wa “Stable Ford” ambapo mshindi atapatikana kwa kuhesabu alama kwenye kila shimo.

 

No comments