Header Ads

test

SERIKALI YAANIKA MIKAKATI KUHAMASISHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA, ORYX WAKABIDHI MITUNGI 700 MKOANI RUVUMA

 Na Mwandishi Wetu,Mbinga


SERIKALI kupitia Wakala wa Nishati Vijijini(REA)kwa mwaka wa fedha 2024/2025,imepanga kutumia zaidi ya Sh.bilioni 10 kwa ajili ya kununua majiko banifu(Gesi) takribani  400,000 ambayo yatasambazwa kwa Wananchi.

Pia imesema lengo la Serikali ni kuongeza matumizi ya Nishati safi ya kupikia nchini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi na kuepusha wananchi kupatwa na maradhi yanayotokana na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa.

Akizungumzawakati akizindua uhamasisha wa matumizi wa nishati safi ya kupikia kwa kutumia majiko banifu ya kampuni ya Oryx Gas kwa wananchi wa wilaya ya Mbinga Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga amesema hadi sasa Serikali kupitia wizara ya nishati(REA) imeshatoa  majiko 83 yenye thamani ya Sh.bilioni 3.5 na kazi ya kugawa majiko hayo inaendelea lengo likiwa ni kupunguza gharama za vifaa vya nishati safi ya kupikia ili wananchi wapate huduma hiyo kwa  gharama nafuu.

Ameongeza Serikali kupitia Wiizarawizara ya Nishati inaendelea kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali ili kuongeza mawakala hadi ngazi ya vijiji ikiwemo kutoa ruzuku kwa mawakala  kupitia miradi mbalimbali.

Kapinga alieleza kuwa,kutokana na jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan,Tanzania imeonekana kuwa kinara wa matumizi ya nishati safi ya kupikia Barani Afrika.

Kuhusu Oryx Naibu Waziri Kapinga ameishukuru Kampuni hiyo kwa namna ambavyo imedhamiria kwa vitendo kuunga mkono juhudi za Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia katika kuhakikisha wananchi wanatumia nishati safi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oryx Gas  Tanzania Ltd Benoit Araman alisema kuwa,zaidi ya Watanzania 33,000 wanapoteza maisha kila mwaka kwa kuvuta moshi na chembechembe zitakonazo na mkaa na kuni,lakini kwa kutumia Gesi ya Kampuni ya Oryx Gesi wataweza kuepukana na tatizo hilo.

Araman alisema,ulinzi wa mazingira kupika kwa kutumia gesi ya Oryx kutazuia ukataji  ovyo wa miti,kwa hiyo itasaidia kulinza mazingira na ukitumia gesi utapika kwa haraka na kwa ufanisi na wanawake watakuwa na muda wa kufanya kazi za kujiletea maendeleo.


Wakati huo huo  Meneja miradi nishati safi ya kupikia wa kampuni ya Oryx Peter Ndomba alisema,kampuni hiyo imeweka mipango yakinifu juu ya namna ya utunzaji wa mazingira sambamba na kutoa elimu kwa wananchi ambayo ni endelevu ili kila mwananchi aweze kupata uelewa juu ya  umuhimu wa nishati safi ya kupikia.

Ndomba amesema hayo jana wakati akikabidhi majiko 300 ya kupikia kwa Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vita Kawawa kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt Samia Suluhu Hassan.

Ndomba alisema,tayari kwa mkoa wa Ruvuma jumla ya majiko banifu 1,000 yametolewa kati ya majiko hayo 700 yamegawiwa wilaya ya Mbinga na 300 wilaya ya Namtumbo lengo ni kusaidia kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi bora ya nishati safi na kwamba zoezi hilo litaendelea katika mikoa mingine hapa nchini.

Mbunge wa jimbo la Namtumbo mkoani Ruvuma Vita Kawawa,amewataka wananchi kuona umuhimu wa kutumia nishati safi na kuacha kutumia nishati ambazo siyo rafiki kwa mazingira.

Mbunge Kawawa alisema hayo wakati wa zoezi la kugawa majiko banifu 300 yenye thamani ya Sh.milioni 25.5 kwa wajasirimali wadogo wakiwemo Mama na Baba lishe kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.






 

No comments