RAIS DK. SAMIA ALIPONGEZA SHIRIKA LA TTCL KUFANIKISHA TAMASHA LA KIZIMKAZI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti cha pongezi Meneja Mkazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL-Zanzibar), Bw. Hillary Mwinyi (kulia) pamoja na Meneja Mkuu wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde (kushoto) kwa kutambua mchango wa TTCL kufanikisha shunguli mbalimbali za Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Kusini Unguja, Zanzibar. |
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekabidhi cheti cha pongezi kwa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kutokana na ushiriki wake wa kipekee katika kufanikisha Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Kusini Unguja, Zanzibar.
Cheti hicho cha pongezi kilipokelewa na Meneja Mkazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL-Zanzibar), Bw. Hillary Mwinyi pamoja na Meneja Mkuu wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL wakati wa hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika Ikulu ndogo Kizimkazi, Zanzibar.
Pongezi hizo ni kutambua mchango wa Shirika la TTCL katika kuunga mkono shughuli za Tamasha la Kizimkazi ikiwa ni pamoja na kufanikisha michezo na shughuli mbalimbali za kijamii, kiutamaduni na kiuchumi wakati wa tamasha kiujumla.
Ushiriki wa TTCL katika tamasha hilo umesaidia upatikanaji wa huduma za mawasiliano kupitia Banda la Maonesho ambalo lilitoa huduma ili kuwezesha wageni na wananchi wa eneo hilo kupata huduma bora. TTCL imeendelea kushirikiana na Serikali na jamii katika kukuza utalii, uchumi, na utamaduni wa Zanzibar.
Cheti hiki cha pongezi ni ishara ya kutambua umuhimu wa TTCL katika kuimarisha maendeleo ya jamii kidigitali na kufanikisha malengo ya kijamii, kiutamaduni na kiuchumi nchini.
Post a Comment