Header Ads

test

Bibi Miaka 70 Kizimbani Kwa kukutwa Na Zaidi Ya Tani Moja Ya Bangi.

 

Yuko Pia Mwanae Na Wenzake Wawili

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv 

BIBI, Felista Mwanri (70), na mtoto wake,  Richard Mwanri (47)  wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na tuhuma za kusafirisha zaidi ya tani moja ya dawa za kulevya aina ya bangi aina ya skanka

bibi Felista na mtoto wake wanashtakiwa pamoja na  Athuman Mohamed maarufu kwa jila la Makame (58) mkazi wa Tanga, Juma Chappa (36) mkazi wa Kiwalani na Omary Mohamed (32) ambae ni dereva anayeishi Buza, Dar es Salaam.


Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa Serikali Eric Davis leo Septemba 10,2024  mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mhini imedai washtakiwa wanatuhumiwa kwa shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya kinyume na sheria.

Imedaiwa, Agosti 28,2024 washtakiwa wakiwa eneo la Tairo Luguruni barabara ya Kwembe ndani ya Wilaya ya Ubungo ǰijini Dar es Salaam walikutwa walisafirisha kilogramu 1815 za dawa za kulevya aina ya bangi.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa kesi inayowakabili ni ya uhujumu uchumi. Wote wamerudishwa mahabusu 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 24,2024 kwa ajili ya kutajwa na kuangalia hatua ya upelelezi ilipofikia.

 

No comments