Header Ads

test

Benki ya Absa Tanzania Yazindua Huduma Iliyoboreshwa ya Prestige Banking ikitoa suluhisho jumuishi za kifedha

Na Mwandishi Wetu


Benki ya Absa Tanzania leo imezindua rasmi huduma yake iliyoboreshwa ya Prestige Banking, kifurushi cha huduma za kifedha chenye mtazamo mpana wa maisha, kilichobuniwa kukidhi mahitaji mbalimbali ya wataalamu na wajasirimali wenye malengo makubwa nchini kote.

 Huduma hii mpya inalenga wataalamu walio katika ajira rasmi wenye kipato cha kati ya Shilingi milioni 2.5 hadi milioni 5.99 kwa mwezi, pamoja na wajasiriamali waliojiajiri, ikiwa na msisitizo mkubwa katika kukuza ukwasi, uwekezaji, na uendelezaji wa biashara. Pia inalenga kuziba pengo linalokua sokoni kwa kutoa suluhisho jumuishi zinazosaidia ukuaji wa kifedha, ustawi wa maisha, na usalama wa muda mrefu.

 Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, alisema huduma hiyo inaakisi dira ya benki inayoweka mteja mbele na kuongozwa na kusudi.

 “Katika Absa, kusudi letu ni kuiwezesha Afrika ya kesho, pamoja… hatua moja baada ya nyingine. Huduma hii ya Prestige iliyoboreshwa, imeundwa kuendana na ndoto halisi za wataalamu na wajasiriamali wa Kitanzania wanaojenga mustakabali wao na kutamani kufika mbali zaidi. Hivi ndivyo tunavyotekeleza kwa vitendo ahadi yetu ya chapa isemayo ‘Stori yako ina Thamani,” alisema Bw. Laiser.

 Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa benki hiyo, Bi. Ndabu Swere, alieleza kuwa huduma hiyo imeundwa mahsusi kuzingatia mitindo ya maisha na matarajio yanayokua ya wateja waliopo kwenye mkondo wa mafanikio.

 “Wataalamu na wajasiriamali wa leo wanatarajia zaidi kutoka kwenye benki zao kuliko huduma za miamala tu. Wanahitaji suluhisho zinazolingana na malengo yao, kusaidia uundaji wa ukwasi, kulinda kile wanachokijenga, na kuboresha mitindo yao ya maisha. Huduma ya Prestige inaleta yote haya kwa pamoja, ikiunganisha huduma rahisi za benki, suluhisho maalum za ukwasi, manufaa ya maisha, na ushauri wa kitaalamu katika kifurushi kimoja cha kiwango cha juu,” alisema Bi. Ndabu.

 Baadhi ya manufaa ya huduma hiyo ni pamoja na  Akaunti ya Prestige inayounganishwa na majukwaa ya kidijitali ya Absa, pamoja na kadi ya Platinum inayotoa urahisi, usalama, na upatikanaji wa taarifa papo hapo.

 Ikitoa suluhisho za  kukuza ukwasi kupitia  Akaunti za akiba za Prestige, amana za muda maalum, mikopo ya nyumba iliyoboreshwa, na kadi za mkopo za Platinum zinazosaidia kufikia malengo ya kifedha yanayokua.

 Huduma hiyo pia hutoa zawadi mbalimbali na manufaa ya Kipekee ya Mtindo wa Maisha kupitia  Programu ya Twin Rewards inayoongeza uwezo wa kupata pointi, ofa za kurejeshewa fedha, punguzo maalum kutoka kwa washirika, pamoja na mikopo  ya magari inayofanya manunuzi ya vitu vya thamani kuwa rahisi zaidi.

 Huduma ya Prestige iliyoboreshwa hutoa pia Suluhisho za Ulinzi kupitia  Bima mbalimbali zinazosaidia kulinda mali, afya, na urithi wa kifedha wa mteja.

 Kupitia huduma hiyo mteja anaweza kupata Ushauri wa kitaalamu ikiwemo uandaaji wa wosia, mipango ya urithi na uendelevu wa mali, pamoja na uwezekano wa kujiunga  na klabu maalum ya afya ili kukuza maisha yenye viwango.

 Benki ya Absa Tanzania imeeleza kuwa huduma hii mpya ni sehemu ya mkakati wake mpana wa kutoa huduma za kifedha zinazomweka mteja katikati, zikivuka mipaka ya bidhaa za kawaida kwa kushughulikia mahitaji kamili ya kifedha na mitindo ya maisha ya wateja.

 “Huduma hii inaonyesha dhamira yetu ya kuwa mshirika wa kifedha anayeaminika katika kila hatua ya maisha ya wateja wetu,” aliongeza Bi. Ndabu. “Kadiri malengo yao yanavyokua, nasi tunakua pamoja nao.”
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa tano kutoka kushoto), akiwa pamoja na maafisa wa benki na wateja, wakishuhudia tukio la uzinduzi rasmi wa Huduma ya Prestige Banking iliyoboreshwa kwa Wataalamu na Wajasiriamali jijini Dar es Salaam jana. Huduma hii imebuniwa kwa ajili ya wataalamu wanaopokea mishahara kati ya TZS milioni 2.5 na TZS milioni 5.99, pamoja na wajasiriamali waliojiajiri, ikiwa na msisitizo mkubwa katika kukuza ukwasi, uwekezaji, na uendelezaji wa biashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, akihutubia wageni waalikwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Huduma ya Prestige Banking iliyoboreshwa kwa Wataalamu na Wajasiriamali jijini Dar es Salaam jana. Huduma hii imebuniwa kwa ajili ya wataalamu wanaopokea mishahara kati ya TZS milioni 2.5 na TZS milioni 5.99, pamoja na wajasiriamali waliojiajiri, ikiwa na msisitizo mkubwa katika kukuza ukwasi, uwekezaji, na uendelezaji wa biashara.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalum wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Thereza Majinge, akitoa ufafanuzi kuhusu Huduma ya Prestige Banking iliyoboreshwa kwa Wataalamu na Wajasiriamali iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jana. Huduma hii imebuniwa kwa ajili ya wataalamu wanaopokea mishahara kati ya TZS milioni 2.5 na TZS milioni 5.99, pamoja na wajasiriamali waliojiajiri, ikiwa na msisitizo mkubwa katika kukuza ukwasi, uwekezaji, na uendelezaji wa biashara.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Swere (katikati), akizungumza na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Huduma ya Prestige Banking iliyoboreshwa kwa Wataalamu na Wajasiriamali jijini Dar es Salaam jana. Huduma hii imebuniwa kwa ajili ya wataalamu wanaopokea mishahara kati ya TZS milioni 2.5 na TZS milioni 5.99, pamoja na wajasiriamali waliojiajiri, ikiwa na msisitizo mkubwa katika kukuza ukwasi, uwekezaji, na uendelezaji wa biashara. 

No comments