Header Ads

test

TPSC YAENDESHA MAFUNZO ELEKEZI KWA WATUMISHI WAPYA TISEZA

Mafunzo Elekezi kwa Watumishi Wapya wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) yameanza leo, Mei 28, 2026, ikiwa ni hatua muhimu ya kuandaa wataalamu wa mamlaka hiyo kwa kuzingatia misingi ya utumishi wa umma na miongozo ya serikali. Watumishi wapya 29 wanashiriki mafunzo haya .yanayotolewa na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC).
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) Bi. Anjela Tulumamanywa, alisema kuwa mafunzo elekezi ni nyenzo muhimu kwa wafanyakazi wapya kujifunza misingi ya utumishi wa umma kupitia miongozo mbalimbali ya serikali. 


"Tunatarajia kuwa baada ya mafunzo haya, mtakuwa watumishi wa umma wanaofuata maadili ya utumishi wa umma, wakiwasiliana kwa ufanisi na kuheshimu usiri wa taarifa na nyaraka za serikali, huku pia wakielewa haki na wajibu wao," amesema.

Kwa upande wake, Bi. Zena Hussein ambaye ni Meneja wa kituo cha mafunzo kwa njia ya Mtandao  akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, amesema kuwa mafunzo haya ni muhimu na lazima kwa watumishi wapya katika utumishi wa umma. 
"Mafunzo haya yanalenga kuimarisha uelewa wa misingi ya utumishi wa umma na miongozo ya serikali, ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa kuzingatia maadili ya kazi," amesisitiza.

Aidha amesema kuwa Mafunzo haya yanatarajiwa kuongeza uelewa wa watumishi wapya kuhusu misingi ya utumishi wa umma na kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ndani ya TISEZA. Vilevile, mchakato huo unazingatia taratibu na miongozo ya serikali, kwa lengo la kuhakikisha majukumu yanatekelezwa kwa uwajibikaji, uadilifu, na ufanisi.
Mafunzo haya ni utekelezaji waraka wa Utumishi Na. 5 wa mwaka 2011, uno wataka waajiri kuhakikisha kuwa watumishi wapya wanapatiwa mafunzo elekezi ndani ya miezi sita tangu kuajiriwa,







 

No comments