TAARIFA YA KUPOTEA KWA FARAJA NICODEMU MWALONGO MIAKA 33
Kwa masikitiko makubwa, familia ya Mr. & Mrs. Boniventura Mwalongo wa Nsalaga, Mbeya, inatangaza kupotea kwa mdogo wao anayefahamika kwa jina la Faraja Nicodemu Mwalongo(33).
Faraja aliondoka nyumbani kwa dada yake, Enilita Ferdinand Mwalongo, eneo la Juhudi, Ilemi – Jiji la Mbeya, saa 2:15 usiku Julai 25, 2026, akieleza kuwa anaelekea Kanisa Katoliki la Roma, Mbeya Mjini. Tangu wakati huo hajarejea nyumbani na hajulikani alipo.
Faraja amekuwa na changamoto ya afya ya akili tangu alipohitimu masomo yake katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), hali iliyomfanya ahitaji uangalizi na msaada wa karibu.
Sifa za mavazi alipokuwa akiondoka:
- Gauni la rangi ya bluu na nyeupe.
- Sweta ya kaba shingo.
- Miguuni alikuwa amevaa mabotiboti.
Familia inaomba kwa dhati ushirikiano wa kila mwananchi katika juhudi za kumtafuta Faraja.
Kwa yeyote atakayemuona Faraja, una taarifa kuhusu alipo, au unadhani umekutana naye, tafadhali usisite kuwasiliana nasi mara moja kupitia namba zifuatazo:
📞 0782 728 605
📞 0756 147 487
📞 0676 003 969
Familia inaendelea kuwa na imani kwamba kwa ushirikiano wa jamii na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, Faraja Nicodemu Mwalongo atapatikana salama na kurejea nyumbani.

Post a Comment