WIZARA YA ARDHI YAPOKEA UJUMBE WA AWALI WA UN-HABITAT KUKAGUA MAANDALIZI YA KUFUNGUA OFISI TANZANIA
Na Munir Shemweta
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imempokea mjumbe maalum kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani (UN-Habitat) kwa ajili ya kukagua maandalizi ya kufunguliwa kwa ofisi za shirika hilo nchini.
Mjumbe huyo maalum, Bw. Grace Lubale, yupo nchini kwa ziara ya siku tatu inayolenga kutembelea na kukagua ofisi zilizotolewa na Serikali ya Tanzania kwa UN-Habitat, ambazo zipo katika jengo la Wizara hiyo lililopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano yaliyosainiwa tarehe 7 Juni 2023 kati ya Serikali ya Tanzania na UN-Habitat, yakilenga kuimarisha ushirikiano katika sekta ya makazi na maendeleo ya miji.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo tarehe 28 April 2026 jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Deogratius Kalimenze, amesema Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha ofisi hiyo inaanza kazi kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja na kutoa vitendea kazi na wataalam wanne watakaosaidia uendeshaji wake.
‘’Serikali ina matarajio makubwa kutokana na uwepo wa ofisi hii, hususan katika kuimarisha juhudi za kushughulikia changamoto mbalimbali katika sekta ya makazi, ikiwemo maendeleo ya miji, matumizi ya nishati jadidifu, ustahimilivu wa miji, pamoja na uboreshaji wa makazi yasiyopangwa’’. ameeleza Bw. Kalimenze.
Kwa upande wake, Bw. Grace Lubale amesema UN-Habitat inaendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali ya Tanzania ili kuhakikisha malengo ya ushirikiano huo yanatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya shirika hilo.
‘’Kupitia ushirikiano huu, maeneo yatakayopatiwa kipaumbele ni pamoja na uboreshaji wa makazi, ujenzi wa nyumba za gharama nafuu pamoja na nishati safi katika majengo’’. amesema,
Ushirikiano kati ya pande hizo mbili pia unalenga kuwezesha upatikanaji wa wadau wa maendeleo na mifumo ya Umoja wa Mataifa katika kusaidia utekelezaji wa miradi ya makazi, pamoja na kuanzisha mifumo madhubuti ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, hususan lengo namba 11 linalohusu miji na makazi endelevu.
Hatua ya kufunguliwa kwa ofisi ya UN-Habitat nchini Tanzania inatarajiwa kuwa chachu ya kuimarisha maendeleo ya sekta ya makazi na miji, na kuongeza ushirikiano wa kimataifa katika kutatua changamoto za makazi nchini.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Deogratius Kalimenze (katikati) akimsikiliza Mjumbe Maalum Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani (UN-Habitat) Bw. Grace Lubale (kushoto) wakati wa kikao kichofanyika katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Makazi Bw. Nicholaus Mwakasege
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imempokea mjumbe maalum kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani (UN-Habitat) kwa ajili ya kukagua maandalizi ya kufunguliwa kwa ofisi za shirika hilo nchini.Mjumbe huyo maalum, Bw. Grace Lubale, yupo nchini kwa ziara ya siku tatu inayolenga kutembelea na kukagua ofisi zilizotolewa na Serikali ya Tanzania kwa UN-Habitat, ambazo zipo katika jengo la Wizara hiyo lililopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano yaliyosainiwa tarehe 7 Juni 2023 kati ya Serikali ya Tanzania na UN-Habitat, yakilenga kuimarisha ushirikiano katika sekta ya makazi na maendeleo ya miji.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo tarehe 28 April 2026 jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Deogratius Kalimenze, amesema Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha ofisi hiyo inaanza kazi kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja na kutoa vitendea kazi na wataalam wanne watakaosaidia uendeshaji wake.
‘’Serikali ina matarajio makubwa kutokana na uwepo wa ofisi hii, hususan katika kuimarisha juhudi za kushughulikia changamoto mbalimbali katika sekta ya makazi, ikiwemo maendeleo ya miji, matumizi ya nishati jadidifu, ustahimilivu wa miji, pamoja na uboreshaji wa makazi yasiyopangwa’’. ameeleza Bw. Kalimenze.
Kwa upande wake, Bw. Grace Lubale amesema UN-Habitat inaendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali ya Tanzania ili kuhakikisha malengo ya ushirikiano huo yanatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya shirika hilo.
‘’Kupitia ushirikiano huu, maeneo yatakayopatiwa kipaumbele ni pamoja na uboreshaji wa makazi, ujenzi wa nyumba za gharama nafuu pamoja na nishati safi katika majengo’’. amesema,
Ushirikiano kati ya pande hizo mbili pia unalenga kuwezesha upatikanaji wa wadau wa maendeleo na mifumo ya Umoja wa Mataifa katika kusaidia utekelezaji wa miradi ya makazi, pamoja na kuanzisha mifumo madhubuti ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, hususan lengo namba 11 linalohusu miji na makazi endelevu.
Hatua ya kufunguliwa kwa ofisi ya UN-Habitat nchini Tanzania inatarajiwa kuwa chachu ya kuimarisha maendeleo ya sekta ya makazi na miji, na kuongeza ushirikiano wa kimataifa katika kutatua changamoto za makazi nchini.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Deogratius Kalimenze (katikati) akimsikiliza Mjumbe Maalum Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani (UN-Habitat) Bw. Grace Lubale (kushoto) wakati wa kikao kichofanyika katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Makazi Bw. Nicholaus Mwakasege

Maafisa wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiwa katika kikao na Mjumbe Maalum Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani (UN-Habitat) Bw. Grace Lubale wakati wa kikao kilichofanyika makao makuu ya wizara Mtumba jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Deogratius Kalimenze (wa pili kushoto) na Mjumbe maalum Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani (UN-Habitat) Bw. Grace Lubale (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa wa Wizara ya Ardhi mara baada ya kukagua ofisi ambazo UN-Habitat inatarajia kuzifungua jijini Dodoma. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

Post a Comment